WAZIRI RIDHIWANI ATINGA MBEYA KUKAGUA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

October 09, 2025


📌 Awakaribisha wananchi kusikia majumuisho yake


Na Mwandishi Wetu, Mbeya


 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu– Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amefika mkoani Mbeya kukagua na kutazama maandalizi ya sherehe za Kuhitimisha Mbio za Mwenge wa uhuru zitakazotanguliwa na Maonyesho ya kazi Mbalimbali na huduma katika Wiki ya Vijana na Kongamano kubwa litakalokutanisha vijana zaidi ya 1500, sinazotaraji kufanyika mjini Mbeya. 

Maonyesho ya Wiki ya Vijana yameanza 8 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba 2025 pamoja na Kongamano la Vijana ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania. 

Shughuli zote zitahitimishwa na sherehe za kilele cha Mwenge wa Uhuru 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dr. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Katika ziara hiyo Ridhiwani amepata nafasi ya Kukagua matayarisho ya shughuli hizo zote na kukutana na wananchi, kuwasalimia na kuwakaribisha kuja kushiriki shughuli hizo zote. 


"Karibuni sana Mbeya, tusikilize Nini mwenge wa Uhuru Umeona," alisema Kikwete.

Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »