PICHA za matukio mbalimbali za Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Soko la Tasaf, Kata ya Nyamwage, Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, leo Alhamisi Oktoba 9,2025.
Katika Mkutano huo Dkt.Nchimbi alimuombea kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu pamoja na Wabunge na Madiwani.
Katika hatua nyingine Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Rufiji,Ndugu Mohammed Mchengerwa na Madiwani.
Dkt.Nchimbi anafikia mkoa wa 19 (Tanzania Bara) akizunguka nchi zima kunadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030,huku akiwahimiza Wananchi kuichagua serika ya CCM kwa miaka mingine mitano,itakayolenga kuwaletea maendeleo Wananchi.
EmoticonEmoticon