NGORONGORO NA TANAPA WAUZA UTALII KWA WADAU WA KIMKAKATI MIJI YA BARCELONA,MADRID NA SEVILLE NCHINI HISPANIA

October 08, 2025


Na Philomena Mbirika, Seville-Hispania

Tarehe 8 Oktoba, 2025 


Maonesho ya Tourism Road Show yaliyoanza tarehe 6 Okoba, 2025  nchini Hispania yamemalizika leo tarehe  8 Oktoba, 2025 katika jiji la Seville, yakihitimisha ziara ya siku tatu iliyofanyika katika majiji ya Barcelona, Madrid na Seville kwa kukutana na mawakala wakubwa wa Utalii kwa lengo la kudani vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji.

Maonesho hayo yaliyowakutanisha mawakala wa safari za kitalii takribani 100 kutoka Hispania yametoa fursa kwa Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kushika Soko la utalii barani Ulaya ambapo ni soko la kimkakati.

Mkurugenzi wa chama cha wakala wa usafiri Hispania Bw. Oscar Gabaldòn  ambaye pia ni mwakilishi wa Tanganyika expedition nchini hapo, alisema kwamba lengo la kuandaa road show hiyo  ni kutokana na mwamko wa watalii nchini hapo kupendelea kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Tanzania.

“Tanzania ni nchi yenye uzuri wa kipekee ambayo imebarikiwa vivutio vya wanyamapori, utamaduni, fukwe nzuri, Milima ya kuvutia ambavyo nyote hivi vinafanya urahisi kwenye Soko la utalii hapa nchini na ndani ya bara la ulaya kwa ujumla” Alisema Oscar

Kwa upande wa washiriki kutoka Ngorongoro na TANAPA wameleza kuwa kupitia maonesho hayo wamepata fursa ya kuuza vivutio vya Utalii pamoja na fursa za uwekezaji zilizo ndani ya maeneo yanayosimamiwa na taasisi hizo kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini na kuwezesha kufikia lengo la taifa la watalii milioni  nane (8) ifikapo mwaka 2030.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »