Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) limefanya ukaguzi na kuridhishwa na kiwango cha maboresho kilichofanywa katika meli ya MV Mwanza iliyofanya safari yake jana tarehe 7 Oktoba, 2025 kutoka Mwanza kuelekea Bukoba.
Akizungumza wakati wa safari hiyo, Mha. Saidi Kaheneko, Kaimu Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa Vyombo vya Usafiri Majini TASAC amesema kwa kuzingatia matokeo ya ukaguzi wa awali, maboresho yaliyofanywa yanaridhisha na hivyo TASAC imeruhusu meli hiyo kufanya safari yake ya kwanza kutoka Mwanza kwenda Bukoba.
“Ukaguzi umefanyika vizuri mapendekezo ya maboresho yaliyotolewa kwenye majaribio ya kwanza yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu yamefuatwa na hivyo, tunathibitisha kuwa MV MWANZA inafaa kuanza safari zake rasmi za kusafirisha abiria na mizigo,” amesema Mha. Kaheneko.
Akizungumzia safari hiyo, Mha. Kaheneko amesema kuwa safari ilifanyika kwa usalama, utulivu na ufanisi mzuri wa uongozaji (navigation) bila changamoto za kiufundi au za kiusalama.
![]() |
Meli hii ya MV Mwanza itafanya safari zake kutoka Mwanza, Kemondo, Bukoba na Port Bell nchini Uganda.
EmoticonEmoticon