WANANCHI WAKARIBISHWA BANDA LA WIZARA YA NISHATI NANENANE DODIMA

August 04, 2025


*📌 Kufahamu fursa na miradi inayoendelea kutekelezwa*



Wizara ya Nishati imeendelea kukaribisha wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Nishati  katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

 Fredrick Marwa, Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati amesema katika maonesho hayo Wizara inaeleza kuhusu  kazi mbalimbal zinaoendelea kufanyika ikiwemo za  utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bonde la Eyasi Wembere.

Marwa amesema wananchi watakapofika katika Banda la Wizara ya Nishati pia watajionea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Wizara  pamoja na Taasisi zake ikiwemo TANESCO, EWURA, REA na TPDC.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »