INEC ITAFANYA KAZI KWA KARIBU NA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI CHOTE CHA UCHAGUZI MKUU 2025

August 04, 2025

 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025 ambapo amewahakikishia washiriki hao kuwa, ofisi yake itafanya kazi nao kwa karibu katika kipindi cha uchaguzi mkuu kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katika vipindi vya redio na runinga na kutoa taarifa kwa wakati. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (Kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile, kabla hajafungua Mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 4, 2025.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (Katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA, Stanslaus Mwita (kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Selemani Mtibora (wa pili kulia), na Mwenyekiti wa Mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari, Lilian Timbuka (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 4, 2025

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »