MCHENGERWA ASHINDA KWA ASILIMIA 99.19 RUFIJI

August 05, 2025

Na Ally Issa

Mgombea wa jimbo la Rufiji anayetetea jimbo lake Mohamed Mchengerwa ameibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha kura za maoni kwa kuzoa asilimia 99.19 ya kura zote zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Prudence Sempa. amesema Mchengerwa amepata kura 8, 465 kati ya kura 8 , 533 zilizopigwa sawa na asili 99.19


Aidha, Sempa amesema kura zote zilizopigwa zilikuwa 8, 534 ambapo idadi ya kura zilizoharibika ni asilimia 0.01 ya kura zote halali.

Wagombea wengine Salma Hamis ,Selemani Mhekela na Hamisa Kisoma waligawana asilimia iliyobaki.

Baada ya kutangaza matokeo hayo wagombea hao wamempongeza Mchengerwa na kuahidi kushirikiana na yeyote kati yao ambaye atachaguliwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) miongoni mwao kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu.

Naye Mchengerwa amewashukuru wajumbe kwa kumpa kura za kishindo huku akisema kuwa ana deni kubwa la kuwalipa endapo Chama chake CCM kitampitisha.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »