NAIBU WAZIRI OWM-TAMISEMI MHE REUBEN KWAGILWA AENDELEA NA ZIARA UBUNGO

December 24, 2025





Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serilali za mitaa TAMISEMI Mhe Reuben Kwagilwa amemtaka katibu Mkuu wa wizara hiyo kuunda timu maalumu ya wataalamu kushughulikia changamoto zilizopo kwenye kituo cha Mabasi cha Magufuli ili kiwe na tija kwa wananchi, wafanyabiashara, Serikali na wadau wengine

Ametoa maelekezo hayo leo Disemba 23,2025 alipofanya ziara kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI kwenye kituo cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Luis Wilayani Ubungo jijini Dar es salaam ambapo amesema miongoni mwa mambo ya kufuatilia ni pamoja na mapato na matumizi ya kituo hicho kero za wananchi,wafanuabiashara wadogo na wadau wengine

Aidha amesema timu hiyo ijimuishe wataalamu kutoka ofisi ua Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wadau wengine lengo likiwa ni kuhakikisha makusidio ya Serikali kutumia fedha nyingi kujenga kituo hicho cha mabasi cha Magufuli linatimia

Akizungimzia suala la mikopo ya asilimia kumi wa vijana wanawake na watu wenye ulemavu jambo ambalo ni miongoni mwa vitu vilivyolalamikiwa na wananchi wa eneo hilo Kwagilwa amewatoa shaka wananchi kuwa Rais Dkt Samia ameshatoa maelekezo hivyo watapata mikopo hiyo

Awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa TAMISEMI kuongea Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando amesema Wilaya hiyo iko shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao

Kwa upande wao baadhi ya wananchi na wadau mbalimbali wamelalamikia suala la mabasi ya mikoani na nchi jirani kutopaki kwenye kituo hicho huku pia wakilalamikia kuchelewa kwa mikopo ya halmashairi

Katika hatua nyingime Naibu Waziri wa TAMISEMI Reuben Kwagilwa ametembelea ujenzi wa daraja na barabara inayoendelea na ujenzi goba mpakani kwa mkorea hadi madale na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili ujenzi huo usiathiriwe na mvua

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »