Na Oscar Assenga,TANGA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Dkt. Juma
Mhina ametoa ahaidi ya kununua kila goli litakalofungwa na timu ya mpira wa
Miguu ya Halmashauri hiyo wa kiasi cha 20,000 ikiwa ni kutoa motisha kwa
wachezaji wa Halmahauri hiyo wanaoshiriki katika Michuano ya Shimisemita
inayoendelea Jijini Tanga.
Aliyasema hayo leo mara baada ya kutembelea timu hiyo kabla ya kuanza
mchezo wa mpira wa miguu dhidi yao na Halmasahauri ya Mpimbwe ikiwa ni michuano ya Shimisemita
inayoendelea kwenye viwanja v ya Shule ya Sekondari Ufundi Mkoani Tanga
Alisema kwamba anaridhishwa na kiwango na mwenendo wa timu hiyo katika
mashindano hayo hivyo akaendelea kutoa hamasa kwao kuhakikisha wanaendelea
kufanya vizuri na kuibuka na ubingwa.
“Hongereni sana mmefanya kazi kubwa sana kwa kuendelea kufanya vizuri
naomba tuendelea kuwa na nidhamu msichoke tupo pamoja na tutaendelea kuwasapoti
“Alisema Mkurugenzi huyo
Hata hivyo aliwataka kuendelea kuhakikisha wanaendelea kupambana ili kuweza kusonga hatua nyengine kwenye mashindano hayo huku akisisitiza nidhamu na kujituma
EmoticonEmoticon