Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa imempitisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MASHILI COMPANY LIMITED ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa (Matinje Mining, Msilale Mining na Igurubi Mining) Ndg Peter Andrea Mashili kugombea Ubunge wa Jimbo la Nzega katika mchakato wa ndani ya chama.
Mashili anachuana na wagombea 6 akiwemo Ndugu Hussein Mohamed BASHE, Regina Maganga NICHOLAUS, James Peter MALOGOTO, Dr. Francis John KIFUTUMO na Eng. Bahati Ntengo NDILLO.
Mashili amabaye hivi karibuni alichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya Ubunge Nzega mjini alisema kuwa ameamua Kugombea Ubunge kwa sababu wananchi wa Nzega wanahitaji nguvu na kasi Mpya ili kuendeleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025-2030.
Alisisitiza kuwa atajikita zaidi katika ushirikishwaji wa wananchi kwenye mambo ya msingi ya maendeleo endelevu, kuwasemea wananchi Changamoto zinaowakabili, kuwapambania ili wanufaike na Fursa zinazotolewa na Serikali hasa katika uendelevu wa sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kwa lengo la Kukuza kipato kwa wananchi ili wajiendeleze kiuchumi na kukuza pato la Taifa.
Peter Mashili ambaye ni mbobezi katika uchimbaji na uuzaji wa madini ni mkazi wa Mtaa wa Mbugani katika Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ni miongoni mwa wafanyabiashara mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania ambao wana historia kubwa katika ushiriki wa shughuli za kijamii hususani uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa katika Jimbo la Nzega wanasema MASHILI wakati wake umefika sasa wa kugombea ubunge wa Jimbo hilo kutokana na kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa wilaya ya Nzega kwa miaka mingi iliyopita na hadi Sasa bado anaendelea kufanya hivyo.
EmoticonEmoticon