DKT.MATARAGIO AITAKA EACOP KUONGEZA KASI UTEKELEZAJI MIRADI YA KIJAMII KWA WANANCHI WANAOPITIWA NA MRADI

July 29, 2025


*📌Lengo ni kuwafanya wananchi kuwa  wa mradi*


*📌 Atembelea  ujenzi wa  kituo  namba 4 cha kusukuma mafuta  Mbogwe na kambi namba 8 ya ujenzi  Bukombe*


📌 *Asifu maendeleo ya mradi na kumtaka mkandarasi kumaliza kazi kwa wakati*


Na Neema Mbuja, Bukombe


Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Mafuta na Gesi Wizara ya Nishati, Dkt James Mataragio, ameelekeza kampuni ya ujenzi  wa bomba la mafuta -EACOP kuhakikisha inaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya huduma za kijamii (Csr activities) kwa kutenga fedha za utekelezaji wa miradi hiyo ili wanqnchi wanaozunguka eneo la mradi kujiona kuwa ni sehemu ya mradi 


Dkt Mataragio ameyasema hayo leo Julai 29,2025 mjini Mbogwe na Bukombe mkoani Geita wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki unaoendelea  kwenye kipande namba 8 pamoja na kituo namba 14 cha kusukuma mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga.

‘’ EACOP mnapaswa kuainisha mahitaji ya kijamii ya wananchi kwenye maeneo husika kama utekelezaji wa huduma za kijamii na kwa mujibu wa matakwa ya utekelezaji wa mkataba ili wananchi wanufaike na miradi ya Maji, Barabara, Shule, Hospitali na huduma zingine za kijamii’’ Amesema Dkt Mataragio

Amesema kwenye maeneo mengj EACOP imefanya vizuri, maendeleo ya mradi yanakwenda vizuri ila kwenye eneo hilo la kurudisha huduma kwa jamii wanapaswa kuliangalia upya na kuja na mpango mkakati wa utekelezaji ili jamii inayozunguka mradi inufaike zaidi.

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo namba 4 cha kusukuma mafuta eneo la Mbogwe, Jihad Diab amesema kwa sasa EACOP inajipanga kutekeleza mkakati wa huduma za jamii CSR ili kusaidia miradi mbalimbali kwenye jamii ambapo kwa sasa wamekwisha ainisha mahitaji ya kila eneo tayari kwa utekelezaji

Amesema ili kuiweka jamii karibu na mradi, wamekuwa na programu za kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mradi na kuwapa fursa viongozi wa vijiji kutembelea eneo la mradi na kuzungumza na wananchi mara kwa mara ili wajione ni sehemu ya mradi

Ujenzi wa bomba la mafuta kipande namba 8 eneo la Bukombe umefikia  asilimia 36  huku eneo la kituo namba 4 eneo la Mbogwe ukkfikia asilimia 46.1

Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki unatekelezwa na nchi mbili za Tanzania na Uganda ambapo kila moja ina hisa asilimia 15, ambapo CNOOC ya China wana asilimia 8 na Total Energies asilimia 62 na mradi unatarajia kukamilika mwezi Julai, 2026.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »