Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Viti vitatu Bara Ndg. Shamira Mshangama @shamiramshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana CCM na kuhamasisha ushiriki wa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.
Shamira alitembelea ofisi ya UVCCM Mkoa wa Shinyanga kufanya kikao kifupi cha ndani, na kukabidhi vifaa vya tehama ikiwemo kompyuta na printa kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Shinyanga iliyopokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo Comrade Benard Benson Werema pamoja na wajumbe wengine ngazi ya mkoa na Wilaya.
Mshangama amekabidhi vifaa hivyo kwa kuirahishia UVCCM mkoa wa Shinyanga katika majukumu ya kutunza kumbukumbu za kazi za umoja wa Vijana.
Akiwa mkoani Shinyanga, Shamira amehudhuria pia Kikao Maalum cha Baraza la UVCCM Mkoani hapo kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Ndg. Benard Werema.
Alipopata nafasi ya kutoa salamu kwenye Baraza hilo Shamira alisisitiza viongozi vijana tunapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya Jumuiya na Malengo ya CCM ya kuendelea kushika dola, huku alikumbusha viongozi vijana kujiimarisha kwa ajili ya kuwa viongozi wakubwa wa baadaye katika Chama na serikali.
EmoticonEmoticon