NA MWANDISHI WETU DODOMA.
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria imepongeza utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoyekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Joseph Mhagama kwa niaba ya kamati leo tarehe 17 machi, 2025, walipotembelea na kukagua miradi ya Ofisi ya waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Jengo la wakala wa mpiga chapa katika eneo la Ilazo jijini Dodoma, Jengo la msajili wa vyama vya siasa pamoja na mradi wa jengo la Kituo cha Taifa cha Mtengamao "National Rehabilitation Center" katika kitengo cha Itega Hospitali ya Milembe.
Akizungumza kwa niaba ya wanakamati, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, amesema wao kama kamati wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuongoza mapinduzi makubwa ya kiutendaji serikalini, hasa katika ujenzi wa miondombinu pamoja na Ofisi za Serikali amabazo zinakwenda kutoa huduma zenye uhakika kwa wananchi wa Tanzania.
Nae Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameishukuru Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria katika kutoa pongezi kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi ambazo zinaendelea kuinua maendeleo ya nchi ya Tanzania.
Mwisho Mhe. Ummy, Nderiananga amewapongeza wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo.
EmoticonEmoticon