KAMATI YA BUNGE YAITAKA REA,TANESCO KUBANDIKA BEI ZA UUNGANISHAJI UMEME KATIKA OFISI ZA SERIKALI ZA VIJIJI

March 17, 2025


*📌 Lengo ni kila Mwananchi kufahamu gharama halisi za kuunganisha umeme*


*📌Kapinga awataka Mameneja REA, TANESCO kuongeza kasi uhamasishaji  wananchi kuunganisha umeme*


📌 *Awahamasisha Wananchi  kupiga  namba 180 wanapopata changamoto ya umeme*



*📍NJOMBE*


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeuagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kubandika gharama halisi za kuunganisha umeme na hatua za kufuata mwananchi akitaka kuunganishishiwa umeme katika Ofisi za Serikali za Vijiji  ili wananchi wazifahamu kwa ufasaha kabla ya kufanya maombi.


Hayo yamesemwa tarehe 17 Machi 2025 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mathayo David katika Kata ya Mang’oto, wilayani Makete mkoani Njombe wakati wa ziara ya kukagua  miradi ya usambazaji wa umeme.

Mhe. Mathayo amesema ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya gharama halisi za kuunganisha umeme ni wakati sasa kwa TANESCO na REA kubandika katika Ofisi za Serikali za Viiji gharama husika pamoja na hatua za kufuata pindi mteja akitaka kuunganishiwa umeme.

“Wananchi wamekuwa wakizungumza tu kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme,  hakuna aliyekuwa  na taarifa sahihi hasa vijijini, hii inawapa hofu wanapohitaji kuunganisha umeme na pia wanapata  ugumu wa kufuata huduma ofisi za TANESCO, wekeni taarifa wazi watu wazijue itaondoa mkanganyiko”, alisisitiza Mhe.Mathayo

Kwa upande wake Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga  amewataka REA na TANESCO kuongeza kasi ya kuwahamaisha wananchi kuungananisha umeme ikiwemo kusuka nyaya katika nyumba zao ili kuunganishiwa umeme hasa wakati miradi inapokuwa inatekelezwa katika maeneo husika ili miradi hiyo inapokamilika wananchi wengi wawe wamepata huduma ya umeme.

Aidha, amewataka wananchi  kupiga simu bure katika  namba 180 ambayo inatoa huduma bure kwa wateja na i kutatuliwa changamoto zao moja kwa moja na kwa haraka.

Katika ziara hiyo Wananchi wa Mang'oto wameipongeza Serikali kwa kuwapelekea  umeme kwani hapo awali walikuwa wakienda Vijiji jirani kufuata huduma mbalimbali ikiwemo kusaga nafaka pamoja na chanjo katika Zahanati zenye Umeme.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng