WAZIRI ULEGA ATETA NA TAFIRI NA ZAFIRI MKUTANO WA SAYANSI NA UVUVI JIJINI ARUSHA

October 30, 2024

 Na Jane Edward, Arusha


 Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdala Ulega ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania kushirikiana na taasisi za kiserikali kuangalia uwezekano wa kupandikiza samaki katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.Ulega ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa tatu wa  Sayansi na Uvuvi viumbe maji amesema ZAFIRI na TAFIRI kufanya utafiti latika eneo la ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika ili kujua idadi ya samaki iliyopo katika maziwa hayo.

Aidha amesema utafiti zaidi ufanyike katika kuangalia uwezekano wa kupandikiza samaki katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere ingawa hatua za mwanzoni zinaonyesha msisitizo mkubwa.

Amesema kuwa wana sayansi wana kazi kubwa ya kufanya juu ya kupatikana kwa chakula cha samaki sambamba na upatikanaji wa vifaranga bora vya samaki ili kuleta matokeo mazuri.

Kwa upande wake Dkt Edwin Mhede Naibu katibu Mkuu anayesimamia Uvuvi ndani ya Wizara ya Mifugo na uvuvi anasema Kupitia taasisi ya mambo ya utafiti kwa kushirikiana na vyuo vikuu pamoja na watafiti kutoka nchi 15 duniani kwa lengo la kufanya maboresho kwenye sekta ya uvuvi na kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi.

"leo tunapokea tafiti mpya kutoka TAFIRI kuona ni wapi kwenye sera zetu tukaangazie tena kwaajili ya kuboresha na matokeo hayo yanaenda kugusa watu takribani milioni sita "Alisema 

Dkt Mary Alphonce Kishe ni mkurugenzi wa uendelezaji utafiti na Uratibu(TAFIRI) anasema mteja wao mkubwa ni serikali na jukumu kubwa la taasisi yao ni kuunganisha tafiti za ukuzaji viumbe maji ambapo wamekutana kupeana uzoefu na kuweka mikakati itakayosaidia ukuzaji wa sekta hiyo.

Amesema kuwa wanaenda kufanya tafiti zitakazotatua changamoto ikiwemo upotevu wa rasilimali za uvuvi baada ya kuvuna ambapo tatizo hili lipo katika sekta hiyo ya uvuvi na kwamba wanaenda kuendeleza tafiti ili kupunguza changamoto zinazoibuka hiyo.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »