Serikali inafanya kila iwezavyo uhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za afya hata pale ambapo watakuwa hawana fedha za kulipia.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameongeza kuwa, Tanzania inafanya jitihada zingine za kuhakikisha vifaa tiba pamoja na madawa ya kutosha sio tu yanapatikana kwa wingi nchini bali pia yanasambazwa katika kila ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji.
Waziri Mkuu Majaliwa alikuwa akizungumza katika Kongamano la Bima ya Afya kwa Wote na Jukwaa la Kitaifa la Ugharamiaji wa Huduma za Afya linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano, Arusha (AICC).
“Kwa sasa jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kuwa magonjwa yote makubwa yaliyokuwa yakitibiwa nje sasa yanapata utatuzi hapa hapa nchini ili kuokoa muda na gharama kwa wagonjwa,” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitaja magonjwa kama ya Moyo na Figo, pamoja na upasuaji mwingine.
“Tunatakiwa pia kuiongezea uwezo bohari ya madawa (MSD) ili taasisi hiyo iweze kuagiza aina zote za madawa na pia kuwa na magari ya kutosha kwa ajili ya kusambaza bidhaa hizo za tiba nchini kote,” aliongeza Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amsema kuwa kwa sasa Madaktari bingwa wa Mama Samia wameanza kuzunguka nchi nzima kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafuata wananchi kila mahali kwa gharama nafuu Zaidi.
“Kwa sasa wamefikia halmashauri karibu zote nchini, huku wananchi zaidi 122,320 wakiwa mamepatiwa huduma na wengine zaidi ya 8,018 wakiwa wamefanyiwa upasuaji mbalimbali kwa mafanikio mazuri,” alisema Waziri Mhagama.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia Maswala ya Afya na Ukimwi, Jackline Kahinja amesema kuwa wanasisitiza kuwa huduma kwa afya kwa wote inakuwa bora na watasimamia vilivyo sheria ya Bima ya Afya kwa wote.
“Tuhakikishe tunafuatilia kwa kina vyanzo vyetu vya mapato ya ndani ili kuwawezesha watu wasio na uwezo waweze pia kupata huduma za afya bila malipo,” alisema Mbunge Kahinja.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Charles Mosses utekelezwaji wa Bima ya Afya kwa wote ni ushahidi tosha kuwa Tanzania inatekeleza kwa vitendo utoaji huduma bora za afya kwa wananchi wake.
“Na kilicho bora zaidi hapa ni kwamba bima hii pia imeweka kipengele maalum cha huduma kwa watu wa chini hususan wale ambao hawana uwezo kabisa wa kifedha,” aliongeza Dk Mosses.
EmoticonEmoticon