Na Oscar Assenga,TANGA.
WAZIRI wa
Michezo,Sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro amepongeza Mashindano ya Oddo
Ummy Cup huku akieleza kwamba watayatumia kuangalia vipaji vya wachezaji na
baadae aone namna ya kumpigia simu Kocha wa timu ya Taifa ili kuona namna ya
kuwapeleka kwenye Taifa ya Taifa.
Dkt Ndumbaro
aliyasema hayo Machi 10 mwaka huu Jijini
Tanga ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Fainali ya Mashindano ya Mpira wa Miguu
ya Oddo Ummy Cup ambayo yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy
Mwalimu kwa lengo la kuibua vipaji vya wachezaji wachanga.
Mashindano
hayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya Lamore Jijini Tanga na yanashirikisha
timu mbalimbali kutoka kwenye Jimbo la Tanga Mjini linaongozwa na Ummy Mwalimu
ambaye pia ni Waziri wa Afya
“Leo
nimekuja Tanga kwa lengo la kuja kuangalia viwango vya wachezaji ili baadae nimpiga
simu kocha wa timu ya Taifa kuona namna nzuri ya kuweza kuwajumuisha kwenye
timu zetu za Taifa”Alisema Waziri Ndumbaro.
Katika
Fainali hiyo timu za Nguvumali na Kiomoni zilitinga hatua hiyo kwa kufanya
vizuri kwa kila mmoja kumtoa mpinzani mwenzake na hivyo kulazimika kukutana
kwenye hatua hiyo ya kumsaka Bingwa ambapo Bingwa alikuwa ni timu ya Kiomoni
“Kwa
heshima ya Waziri Ummy Mwalimu nimeacha shughuli zote nimekuja Tanga mimi
Waziri wa michezo ili niweze kuona vipaji vilivyopo hapa Tanga kwa maana
historia ya mpira ni kubwa na nimeambiwa Juma Mgunda yupo hapa hivyo tunaweza
kutumia mashindano haya kupata wachezaji wa timu ya Taifa”Alisema Waziri
Ndumbaro.
Akubali Ombi la Mbunge Ummy
Katika
hatua nyengine Waziri Ndumbaro amekubali ombi la Mbunge Ummy Mwalimu ambaye alimuomba
atafute shule mmoja mkoani humo waifanye kuwa ya vipaji vya michezo.
Akijibu
Ombi hilo Waziri Dkt Ndumbaro alisema kwamba yeye akisema wataona namna ya
kwenda kulitekeleza ili uwepo wa shule hiyo uweze kupatikana mkoani Tanga.
“Mh Ummy
nimepokea ombi lao wewe ukisema mimi ni utekelezaji tu hivyo nitakwenda
kulifanyia kazi”Alisema
Mwisho
EmoticonEmoticon