Na Mwandishi Wetu - Dar es salaam
Kampuni ya kutoka China ya CRJE (East Africa) Ltd imejivunia uwekezaji wake mkubwa katika Mradi mkubwa wa jengo la kibiashara Peninsula Noble Center, ambapo umekuwa moja ya miradi mikubwa ya maendeleo ya Kampuni hiyo nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wakati wa utoaji tuzo kwa wafanyakazi bora wa Peninsula Noble Center na Victoria Noble Centre katika hafla aliyowakutanisha wadau mbali mbali jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kituo cha Uendeshaji na Usimamizi wa Mali za CRJE, Bw. LI TIANYE, alisema kuwa mradi huo unaonyesha dhamira yao ya muda mrefu ya ujenzi wa hali ya juu, uendeshaji sanifu, na maendeleo endelevu.
"Lengo letu ni kuunganisha teknolojia za ujenzi za Kichina na mfumo wa kisheria, mazingira ya soko, na muktadha wa kitamaduni wa Tanzania," alisema Bw. LI TIANYE.
Alisema kuwa kituo cha Peninsula Noble ni mradi muhimu uliotengenezwa na CRJE, baada ya Nyerere Foundation Square na Victoria Noble Centre, kama sehemu ya maendeleo yake ya kimkakati nchini Tanzania.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema katika kipindi chote cha ujenzi na uendeshaji wa mradi huo, CRJE wamezingatia viwango vya juu katika ujenzi wa majengo, wametumia mifumo bora katika uendelezaji wa majengo na kuendelea kujenga majengo yanayoendana na hali ya soko la Tanzania.
"Lengo letu limekuwa kuunganisha ipasavyo teknolojia ya ujenzi iliyothibitishwa ya China, uzoefu wa usimamizi, na viwango vya huduma na mfumo wa kisheria wa Tanzania, mazingira ya soko, na muktadha wa kitamaduni. Kupitia mawasilisho ya leo, mijadala, na ziara za kutembelea jengo hili, tunatumai watu wengi watapata kujifunza ubora wa ujenzi tunaofanya, falsafa ya uendeshaji, na mfumo wa huduma zitolewazo katika Kituo cha Noble cha Peninsula."
Alisisitiza: "Wakati huo huo, tunaweka umuhimu mkubwa katika kusikiliza maoni na mapendekezo ya wadau wetu, washirika, na timu za usimamizi wa mali. Kiini cha uendeshaji wa mali kiko katika huduma, na uboreshaji pamoja na usimamizi unategemea uelewa, msaada, na ushiriki wa ninyi nyote."
Msimamizi wa Mali wa Kituo cha Peninsula Noble, Bi. Jackline Charles, alieleza kuwa kituo hicho kina maduka 6 kwenye ghorofa ya chini, ikiwa ni pamoja na Supermarketi ya Kimataifa, Kampuni ya Bima, Biashara ya Fedha za Kigeni, Duka la Vito, Mgahawa, Whisky Hub, na Duka la Mapambo ya Nyumbani.
Ofisi za kawaida ziko kutoka ghorofa ya 2 hadi ya 7, zikiwa na muonekano mzuri wa bahari na mandhari ya kuvutia katika eneo la Masaki.
Jengo la Peninsula Noble lina jumla ya nafasi 222 za parking, 103 zikiwa kwenye eneo la chini ya ardhi na 119 kwenye eneo la nje.
Alasema kuwa Jengo la Peninsula Noble lina mfumo wa usalama wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kamera za CCTV, mfumo wa kuzuia moto, na walindi wa usalama.
Tukio hilo la Peninsula Noble Centre Project Open Day liliwashirikisha wageni zaidi ya 200, ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali, wataalam wa sekta, na wafanyabiashara.
Jengo hilo la Peninsula Noble linatarajiwa kutengeneza nafasi za kazi zaidi ya 500 na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi ya Tanzania.
Kampuni ya CRJE inaendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ya mali isiyohamishika nchini Tanzania, na jengo ka kibiashara la Peninsula Noble Centre ni moja ya miradi yake mikubwa.
Akizungumza kwa niaba ya wateja wengine wa Noble Centre Penisular, Mmoja wa maofisa kutoka Kampuni ya GIG Consult Bi Lorna Mbwette alisema, "Kampuni yetu ambayo imepanga katika jengo hili inashughulika kutoa huduma za ushauri wa kisheria, rasilimali watu na biashara kwa makampuni ya ukubwa wote ili kuwasaidia kufikia malengo yao. Tunaipongeza CRJE kwa kuendeleza mradi huu wa hali ya juu unaoshughulikia changamoto za mazingira na biashara katika jiji la Dar es Salaam."
Lorna aliongeza, "Kama washauri wa masuala ya sheria na biashara, tunaweza kuona jinsi mradi huu utakavyowezesha ukuaji wa biashara zetu na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania. Tunathamini ushirikiano mzuri na CRJE na tunaamini kuwa kwa pamoja tunaweza kufikia malengo yetu ya pamoja."










EmoticonEmoticon