WADAIWA KODI YA ARDHI KIKAONGONI

December 23, 2025


 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Masasi wakati wa ziara yake wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

Sehemu ya watumishi wa halmashauri ya Masasi mkoani Mtwara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo wakati wa ziara yake wilayani humo (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Sehemu ya watumishi wa halmashauri ya Masasi mkoani Mtwara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo wakati wa ziara yake wilayani humo (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


 Waziri Akwilapo Ataka Kukamilisha malipo ifikapo Desemba 31, 2025



· Aagiza Vituo vya Makusanyo ya Kodi kutoa huduma bora



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameelekeza wadaiwa wote wa Kodi ya Pango la Ardhi nchini wawe wamekamilisha malipo ya madeni yao kufikia Desemba 31, 2025.



Akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Masasi mkoani Mtwara leo tarehe 23 Desemba 2025 Mhe. Dkt Akwilapo amesema, kuchelewa kulipwa kodi ya pango la ardhi kutasababisha wamiliki wa ardhi kuwa na malimbikizo ya madeni pamoja na riba.



Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, madhara mengine yanayoweza kutokea kwa wamiliki ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kufutiwa umiliki wa ardhi. Hatua hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya ardhi Sura ya 113 Fungu la 48 (1), 50, 51 na 52.



Mhe. Dkt Akwilapo ameelekeza vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi katika ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri nchini kuhakikisha vinatoa huduma bora za kuwasaidia wananchi wanaopata changamoto za kulipa kodi hiyo kwa kuzingatia utu pale wanapotekeleza majukumu yao.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »