KAMATI YA SIASA YA CCM MKOA WA TANGA YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI MUHEZA.

November 09, 2023

Mjumbe wa kamati hiyo Ndugu, Omari AyubuW wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga akizungumza wakatiwa ziara hiyo

 







Kamati ya Siasa Mkoa wa Tanga ikiongozwa na Mjumbe wa kamati hiyo Ndugu, Omari Ayubu imetembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Muheza Mjini unaosimamiwa na TANGA UWASA.


Akisoma taarifa ya mradi kwa viongozi na wajumbe wa ziara hiyo, Mhandisi Violet Kazumba kutoka kitengo cha Miradi amesema kuwa, Utekelezaji wa mradi huu ni muendelezo wa miradi ambayo imetekelezwa katika eneo la Muheza mjini lengo kuu ikiwa ni kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi, ambapo mradi huu unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 11,000 katika maeneo ya Tanganyika, Kwemkabara na Masuguru ambao kwa sasa wanapata huduma ya maji kwa mgao.


"Mradi unagharama ya Shilingi Mil.638 na unatekelezwa kwa njia ya mfumo wa Force Acount, ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 80 na baadhi ya wananchi wa maeneo husika wameanza kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma ya maji kupitia vituo saba (7) vya kuchotea maji vilivyojengwa na kukarabatiwa katika maeneo mbalimbali" Alisema Mhansi Kazumba.


Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa na kukagua mradi huo Mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Tanga Ndugu, Omari Ayubu ameipongeza TANGA UWASA kwa kazi nzuri inayoendea kufanyika katika kuhakikisha wananchi wa Muheza wanapata huduma ya majisafi.


"Nawapongeza wenzetu wa TANGA UWASA kwa kazi nzuri na jitihada zao katika kuhakikisha wananchi wanapata maji na niwatake wananchi tuwe walinzi wazuri wa miundombinu ili tufanikishe upatikanaji wa huduma nzuri na kwa wakati wote", alisema.


Kamati ya Siasa Mkoa wa Tanga inafanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo lengo ni kuhakikisha ilani ya chama cha mapinduzi inatekelezwa na wananchi wanapata huduma pasipo changamoto yoyote.





Share this

Related Posts

Previous
Next Post »