WANAFUNZI 500 JIJINI TANGA WASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA MICHEZO PLUS .

January 30, 2026



Na Oscar Assenga, TANGA



BONANZA la Michezo maarufu kama Michezo Plus limekuwa na mvuto wa aina yake huku likifanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Tanga Ufundi kwa kushirkisha wanafunzi zaidi ya 500.


Wanafunzi hao kutoka shule 50 Jijini Tanga ambao walishiriki katika Michezo ya Mpira wa Miguu,Pete na Wavu huku wakionyesha vipaji vya hali ya juu hatua iliyoshangiliwa na wadau wa michezo ambao walijitokeza kushuhudia bonanza hilo


Akizungumza baada ya kumalizika kwa Bonanza hilo Afisa Michezo wa Jiji la Tanga na Mratibu wa Michezo Plus katika mradi unaotekelezwa na Jiji hilo ukifadhiliwa nan a Botnar Foundation chini ya Programu ya Tanga Yetu Lucy Michael alisema kwamba waliliandaamaalumu kwa ajili ya kujenga mahusiano na kuwajenga kiakili.

Alisema kwamba bonanza hilo litakuwa linafanyika kila mwaka mara mbili ambapo hilo limeanza kwa kufungua mwaka na kukaribisha wanafunzi na watafanya bonanza la vijana.



Awali akizungumza Mratibu wa Bonanza hilo Haji Milao alisema kwamba nia na madhumuni yake ni kuwaweka watoto sawa kwa ajili ya michezo ya Umistashumta mwaka huu 2026 ikiwemo kutengeneza afya za watoto ili waweze kuwa sawa na watoto wakiwa vizuri kwenye michezo hata darasani watakuwa vizuri.



Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Makorora Zuhuru Ally alisema michezo hiyo ina faida kubwa sana kwao kutokana na kwamba inawafanya wakutana na wenzao na kubadilisha mawazo jambo ambalo linawapa fursa.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »