Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro
MKUU wa Wilaya ya Same Kasilda mgeni ameendelea na ziara zake kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo akiwa Kata ya Njoro amepokea kero ya ubovu wa barabara, kukosekana kwa nishati ya umeme kwenye baadhi ya Vitengoji pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.
Mgeni amepokea kero hizo wakati wa mkutano wa hadhara wa wakazi wa kata hiyo uliofanyika katika Kijiji cha Emuguri ambacho asilimia kubwa ya wakazi wake ni wafugaji ambapo walitumia mkutano huo kuwasilisha kero hizo.
Akitolea ufafanuzi hoja hizo mkuu huyo wa Wilaya amesema tayari Serikali ya imeshatoa zaidi ya Sh.bilioni tisa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwenye Wilaya ya Same na miongoni mwa barabara zilizo kwenye mpango wa matengenezo ni barabara kutoka makao makuu ya kata hadi kwenye kijiji hicho cha Emuguri ambayo ipo kwenye bajeti ya mwaka huu 2023/2024 ambayo muda wowote itaanza kutengenezwa.
Upande wa nishati ya Umeme wananchi walihoji kuwa baadhi ya vitongoji kwenye kata hiyo havina umeme, ambapo kwa mujibu wa wataalam vitongoji vyote vipo kwenye mpango wa kufikishiwa umeme kwa bajeti ya mwaka huu ambapo serikali emetenga zaidi ya shilingi Milion 700 atika baejeti ya mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na miradi ya Umeme kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 maeneo yote ya Wilaya ya Same yemefikiwa na huduma.
Kuhusu maji safi amesema Serikali imeanza taratibu za kutaka kuchimba kisima kikubwa kupunguza changamoto iliyopo pia kijiji hicho cha Emuguri ni kati ya vijini 16 vya wilaya ya Same vitakavyo nufaika na mradi mkubwa wa Same, Mwanga-Koroge ambao kwa awamu ya kwanza utakamilika Juni mwakani mradi huo utagharimu zaidi ya shilling Milion 137.
“Kwa niaba ya wakazi wa Same tunamshukuru Sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutujali wananchi wake na kuridhia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na sisi wasaidizi wake ahadi yetu ni kuimarisha usimamizi kuhakikisha fedha zote zinazo tolewa na serikali zinatumika kama ilivyoekusudiwa kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyo kubalika."
Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wakazi wa Same kuwa walinzi wa miundombinu inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu,na kusisitiza pia utunzaji wa mazingira hasa maeneo ya vyanzo vya maji.
EmoticonEmoticon