PANGANI KUJA NA MKAKATI WA UFUMBUZI WA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU WA WANAFUNZI

September 04, 2023

Mkazi wa Kijiji cha Kwakibuyu Ramadhan Mohammed akiwasilisha mada katika mafunzo ya kuwajengea ujuzi wa uhamasishaji jamii katika utetezi wa utatuzi wa changamoto za kielimu kwenye vijiji vya Mkaramo,Ubangaa,Mkwajuni,Kwakibuyu,Kipumbwi na Stahabu.mafunzo hayo yaliendeshwa na asasi ya Tree of Hope chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS)



Pangani Kujenga maelewano baina ya wazazi,wananchi,walimu ,viongozi na wanafunzi  imeelezwa kuwa ndiyo ufumbuzi wa kuongeza kiwango cha ufaulu wa  mitihani ya kitaifa kwa wanafunzi Wilayani Pangani.

Wajumbe wa kamati ya kuhamasisha uwajibikaji jamii na mamlaka zinazohusika kuboresha elimu katika vijiji vya Kipumbwi, Mkalamo,Ubangaa na Stahabu walisema hayo walipokuwa wakizungumza

Wajumbe hao ambao walikuwa wakizungumza baada ya  mafunzo elekezi ya utekelezaji wa mradi wa kujamasisha jamii na mamlaka zinazohusika kuboresha elimu katika jamii unaosimamiwa na asasi isiyo ya kiserikali  ya Tree Of Hope chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society (FCS) walisema wanakwenda kutumia kila mbinu sahihi kuhakikisha maelewano yanajengeka kwa sababu wamebaini ndiyo kiini cha mafanikio.


Ali Ibrahim wa Kijiji cha Kwakibuyu ambacho wanafunzi wake wanasoma shule ya msingi Kipumbwi Wilayani hapa alisema badala ya kutupiana lawama ufaulu utapatikana kwa Kujenga maelewano na kuwa kitu kimoja katika kutekeleza majukumu.


"Ipo changamoto ya utoro,uhaba wa walimu na baadhi ya shule kukosa maji..kila changamoto ina njia zake wazazi wakichangia vyema vyakula wanafunzi watavutika na hawatatoroka,lakini uhaba wa walimu wazazi wakichangia kuwalipa posho walimu wastaafu ufaulu utaongezeka" alisema Ali.


Mratibu wa mradi huo kutoka Tree of Hope,Goodluck Malilo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa mbinu wajumbe wa kamati hizo za utatizi wa changamoto za kielimu kwenye maeneo ya vijiji hivyo ili kuboresha elimu na kuinua kiwango cha ufaulu.


"Changamoto za kielimu katika vijiji vingi zunajulikana na kila mwananchi,

 mamlaka na walimu na uwepo wake siyo kwa sababu wenye mamlaka wameshindwa kuzitatua bali zimekosa utetezi na hili ndilo jukumu la wanakamati" alisema Malilo.


Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah  alisema kamati hizo zinasaidia kuwezesha kila mmoja kuona uchungu na maendeleo ya elimu na kutimiza wajibu wake.


 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »