TANGA UWASA YATUMIA MILIONI 20 KUKARABATI MTANDAO WA MAJI TAKA USAGARA

September 04, 2023

 

Meneja wa Mazingira wa Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani akikagua mtandao wa maji taka katika eneo la Usagara Jijini Tanga ambao wameufanyia ukarabati mkubwa
Meneja wa Mazingira Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani akikagua mtandao wa maji taka katika eneo la Usagara Jijini Tanga ambao wameufanyia ukarabati mkubwa
Muonekano wa chemba zilizokarabatiwa
Muonekano wa chemba zilizokarabatiwa


Na Oscar Assenga, TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imetumia milioni 20 kwa ajili ya kuukarabati mtandao wa maji taka wa zamani katika eneo la Usagara maarufu kama Bandari Chafu.

Akizungumza Meneja wa Mazingira wa Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani alisema uamuzi wa kuukarabati mtandao huo wa maji taka waliufanya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa wa eneo hilo tokea 2018.



Alisema malalamiko hayo yalikuwa yanahusiana na miuondombiu ya maji taka eneo hilo kuwa chakavu na hivyo kuhatarisha afya zao na hivyo kuomba mtandao huo uliojengwa na TPA miaka ya nyuma na hivyo baada ya kubinafishwa nyumba hizo.



Alisema hivyo wanawaomba Tanga Uwasa iwarebishie mfumo huo ambapo awali ulikuwa baada ya kuona changamoto hizo waliamua watenge fedha Milioni 20 kwa ajili ya kuukarabati mtandao huo.



Alisema katika ukarabati wa mtandao huo ulihusisha ukarabati wa chemba kubwa ambazo zinapokea maji taka kutoka kwenye maeneo hayo na ukarabati wa chemba ndogo ndogo ambazo zinaunganisha bomba na bomba na maeneo yenye bomba chakavu .



“Hayo ndio maeneo tuliyoyakarabati na tunatarajia kukarabati na mwaka huu tutakamilisha mpango huo wa ukarabati kukamilisha mfumo hiyo ili kuuwezesha kuishi muda mrefu hiyo itasaidia kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza”Alisema



Hata hivyo alitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuhakikisha miundombinu ya maji taka kuhakikisha hawaweki taka ngumu na wanaitunza ili iweze kukaa muda mrefu


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »