BALOZI CP KAGANDA AKUTANA NA MEJA JENERALI MNKANDE

December 04, 2025

 


Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP - Suzan Kaganda, amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa wa Wakuu wa Vyuo vya Ukamanda na Unadhimu Afrika (African Conference of Commandants-ACOC) Meja Jen. SJ Mnkande.

Meja Mnkande ni Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti-Arusha, na anaongoza ujumbe kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao upo jijini Harare kuanzia tarehe 01 hadi 05 Disemba, 2025, Zimbabwe kushiriki warsha ya  mafunzo ya 17th ya utayari wa Jeshi la Afrika (African Standby Force) kwa lengo la kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AU) katika kusimamia na kulinda kikamilifu mipaka ya nchi zao na kukabiliana na uhalifu unaohatarisha amani Barani Afrika.

Warsha hiyo pia inatumika kama jukwaa la ukusanyaji michango ya mawazo kutoka kwa nchi washiriki na wadau wengine kuandaa mafunzo ya utayari wa Jeshi la Afrika (African Standby Force) na mapitio ya miongozo ya mafunzo ya kila mwaka kwa vipindi vijavyo.



Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »