RAIS SAMIA AOMBWA KUIPA NGUVU ZAIDI SHERIA KWA WANAOFANYA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO

September 25, 2022

 


Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia  ya Tanga Youth Talent Asociation( Tayota)  George Bwire akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utekelezaji wa mradi wa kupiga vita ukatili wa kijinsia aina zote kwa  watoto na vijana wa rika balehe uliofanyika kwenye shule ya msingi na Sekondari kata ya Kirare ambapo Mradi huo unatekelezwa katika Kata zote za Jiji la Tanga na mitaa wenye lengo kupambana na ukatili ambao watoto wadogo na vijana wanaopitia na unafadhiliwa na Botnar Foundation kutoka Uswis.
Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia  ya Tanga Youth Talent Asociation( Tayota)  George Bwire akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utekelezaji wa mradi wa kupiga vita ukatili wa kijinsia aina zote kwa  watoto na vijana wa rika balehe uliofanyika kwenye shule ya msingi na Sekondari kata ya Kirare ambapo Mradi huo unatekelezwa katika Kata zote za Jiji la Tanga na mitaa wenye lengo kupambana na ukatili ambao watoto wadogo na vijana wanaopitia na unafadhiliwa na Botnar Foundation kutoka Uswis.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Kirare 


 Na Oscar Assenga,TANGA.


Rais Samia Suluhu ameombwa kuangalia namna ya kuipa nguvu zaidi sheria ya watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto kuweza kushughulikiwa kikamilifu hatua itakayowezesha kukomesha vitendo hivyo kwenye Jamii.

Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki  na Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia  ya Tanga Youth Talent Asociation( Tayota)  George Bwire wakati wa utekelezaji wa mradi wa kupiga vita ukatili wa kijinsia aina zote kwa  watoto na vijana wa rika balehe uliofanyika kwenye shule ya msingi na Sekondari kata ya Kirare.

Alisema sheria zipo wazi ikiwemo zile ambazo zinawalinda watoto na utekelezaji wake unafanyika vizuri lakini kumekuwa na mapungufu ya kibinadamu kwa watu kwenye vyombo husika ikiwemo mahakamani na Jeshi la Polisi lakini kwa mujibu wa sheria zipo na zinajitosheleza na utekelezaji inabidi ufanyike kwa hali ya ukamilifu.

Mradi huo unatekelezwa katika Kata zote za Jiji la Tanga na mitaa wenye lengo kupambana na ukatili ambao watoto wadogo na vijana wanaopitia na unafadhiliwa na Botnar Foundation kutoka Uswis.

"Nikikuta na Rais Samia Suluhu nitamwambia azidishe nguvu sheria  watu wanaowatendea watoto ukatili waweze kushughukiwa kikamilifu na sio mtu anawafanya ukatili lakini anaonekana mitaani anazunguka hii sio sawa hivyo waweze kushughulikiwa bila upendeleo"Alisema


Mkurugenzi huyo alisema mradi huo kwa sasa unatekelezwa na asasi mbili ambazo  ni Tayota na Tree of Hope na wamefikia shule zote za Tanga 81 za msingi na 25 za Sekondari kwa ujumla wanafunzi waliofikiwa ni 49,000 huku akieleza lengo la mradi kwa awali  ni kuwafikia wanafunzi 10,000. 

Alisema  lakini wameenda mbali zaidi kuwafikia wanafunzi wote wanatoa elimu ya kuwajengea uelewa juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia maana wengine hawafahamu kwamba kuna vitu wanaweza kufanyiwa ni viashiria vya ukatili hivyo ni fursa nzuri kwao kufika shuleni kuweza kuwajengea uelewa.

"Lakini zaidi ya hapa tumekwenda  kwenye Jamii maana wengine wanaowafanyia vitendo vya ukatili ni wana Jamii wanashughu hivyo tunaungana nao  jioni kwenye mitaa kuhamasisha wawalinde watoto lakini kukomesha visa vya ukatili na Jamii za Tanga kulinda maana hilo jambo unakuta limefanywa na mjomba  baba mdogo kwa sababu wanataka kulindana kifamilia mtoto akakoshwa haki na hivyo vitendo vipi sana"Alisema Mkurugenzi huyo 

Hata hivyo alisema kwa sasa wapo kwenye harakati za kuundaa ripoti kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na idara ya ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii ili waweze kufanya uchunguzi zaidi na ambao utasaus kywashughuloliwa wanaotumiwa kwa Mujibu wa sheria

Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo alisema asilimia 60 ya vitendo vya ukatili majumbani vinachangiwa na ndugu wa karibu na hivyo kushindwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili kuweza kuvikomesha vitendo hivyo kwenye Jamii .


"Kabla ya kuanza kutekeleza mradi huu tulifanya utafiti tatizo hilo tulipitia ripoti ya hivi karibuni kutoka Ofisi ua DCI kwamba Tanga ni mkoa wa Tatu kwenye ukatili na inaonyesha watoto wanapitia hali ngumu za mateso, watoto wadogo kuanzia darasa la Pili  na kuendelea wanaathirika sana na vitendo vya ukatili"Alisema 

Awali akizungumza wakati wa semina hiyo Emanuel Elias alisema wamefikia kutoa elimu ya kupiga vita ukatili kwa watoto namna ya kujua athari na aina ya namna ya kuweza kuepukana nayo pindi wanapokutana nayo.

Alisema wamelazimika kutoa elimu kutokana na matukio mengi yaliyoshamiri katika Jiji la Tanga shule nyingi walizotembelea mwanzl wamegundua upo ukatili wa aina  nyingi ambao watoto wanafanyiwa majumbani hasa wa kingono na kimwili.

Alisema lengo lao nikwenda shule zote bila kubagua ilo kupata visa mkasa na kupata elimu ya ukatili huku akiitaka Jamii hususani familia kutilia mkazo malezi Bora kwa watoto maana hayo yote chanzo chake ni kukosekana kwa malezi Bora kwenye Jamii.

Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kirare Erick Mzungu elimu walioipata itawasaidia pindi watakapoona vitendo vya ukatili vinafanyika ili waweze kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kuweza kutatuliwa na Jamii iweze kubaki Salama dhidi ya vitendo hivyo.

Alisema kwamba kupitia elimu hiyo wamegundua namna wanaweza kutoa taarifa ya kuhusu vitendo hivyo vya ukatili ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua ikiwemo kuvikomesha .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »