TWANGA PEPETA KUWASHA MOTO HARBOURS CLUB MKESHA WA KUUKARIBISHA MWAKA 2026

December 30, 2025

 



Na Mwandishi WETU, TANGA.

BENDI ya Mziki wa Dansi ya Twanga Pepeta inatarajiwa kuwasha moto mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 katika ukumbi wa Harbours Jijini Tanga.

Akizungumza na Mtandao huu Katibu Mtendaji wa Harbours Club Athumani Mkumba maarufu kama Senetor alisema kwamba maandalizi yanaendelea vizuri na yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Alisema kwamba wasanii wanaounda bendi ya Twanga Pepeta wanatarajiwa kuwasili Jijini Tanga Desemba 31 mwaka huu tayari kwa ajili ya kujiandaa na Onyesho hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na umahiri wa bendi hiyo.

“Nitoe wito kwa wakazi wa Jijini la Tanga na viunga vyake kujitokeza kwa wingi katika onyesho hili kwa sababu litakuwa la aina yake kutokana na namna wasanii hao walivyojipanga kutoa burudani kwao “Alisema .

Alisema kwamba viingilio ambavyo wameviweka ni daraja la kawaida (Regular) Tsh 10,000/= na VIP Tsh 20,0000/= ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi na wapenda burudani katika mkoa huo waweze kupata burudani ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii “Alisema

Hata hivyo alisema wameamua kuileta bendi hiyo baada ya kufanya tathimini wakagundua Twanga Pepeta inaweza kukata kiu ya burudani kwa wanachi na wakazi wa mji wa Tanga. Aidha katika kupamba burudani hizo zitasindikizwa na Bendi ya Mkoa wa Tanga -The Miracle Band (Wavuvi wa Pwani)


Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »