Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia
ameunda Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa
2017/18.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Ahmed Mgoyi wakati Makamu
Mwenyekiti ni Almas Kasongo ilihali Amiri Mhando ameteuliwa kuwa Katibu
wa kamati hiyo ya tuzo.
Mhando ni Mhariri wa Gazeti la Spotileo linalotolewa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali - Tanzania Standard Newspaper (TSN).
Wajumbe ambao wameteuliwa ni Ibrahim Kaude; Mkuu wa Kitengo cha
Michezo katika Kampuni ya Azam Media, Patrick Kahemele na Kocha mkongwe
wa soka, Kenny ‘Mzazi’ Mwaisabula.
Kadhaika Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji ya Global (Global
Publisher inayochapisha magazeti kadhaa likiwamo Championi), Saleh
Ally; Mtangazaji mahiri wa michezo kutoka Kituo cha Redio cha EFM,
Ibrahim Masoud na Mtangazaji wa Vipindi katika Kituo cha Radio ya Watu,
Fatma Likwata.
Pia wamo Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Gazeti la Mwanaspoti
linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communication (MCL), Gift Macha;
Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu, Said George na
Mhariri wa Michezo wa Gazeti la HabariLeo linalotolewa na TSN, Zena
Chande.
EmoticonEmoticon