Maafisa
wa Mfuko wa PSPF kulia Faidha Khatau na Hazina Konde wakimkabidhi
mashukaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Ali Salum
Ali anayefutia ni Mkurugenzi Utawala na Uendeshaji Dr. Abubakar Khamis
Hamadi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa jengo jipya wa Hospitali
ya Watoto Mnazi mmoja PSPF imekabidhi mashuka 75 kwa ajili ya wodi za
watoto katika hospitali hiyo Kuu Zanzibar ikiwa ni moja ya kusaidia
Jamii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali
akipokea mashuka kutoka kwa Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi
Hazina Konde (katikati) na Afisa Mkuu wa Tawi la Zanzibar PSPF Bi.
Faidha Thatau wakikabidhi mashuka hayo kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya
Watoto katika hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Zanzibar hafla hiyo
imefanyika katika majengo mapya wa hospitali hiyo Zanzibar.
Afisa
Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Faidha Thatau akizungumza
wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi mashuka kwa Uongozi wa Hospitali Kuu
ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mfuko wa PSPF hutowa huduma za mafao mbalimbali
kwa Wanachama wake Bima ya Afya kwa wateja wao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali
akitowa shukrani kwa Uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao huo na
kuwataka isiwe mwisho iwe ni endelevu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa
hospitali hiyo uwezo ukiruhusu.
Afisa
Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Bi. Faidha Khatau akigawa vipeperushi vya
maelezo ya PSPF kwa viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kujuwa huduma
zinazotolewa na Mfuko huo.
Viongozi
wa Hospitali ya Mnazi Mmoja wakifuatilia vipeperushi vya Mfuko wa PSPF
baada ya kukabidhiwa kupata maelezo ya PSPF, wakati wa hafla ya
kukabidhi msaada wa mashuka kwa ajili ya Wodi ya Watoto Zanzibar.
Afisa
Mfawidhi Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar kulia Bi Faidha Khatau
akimkabidhi mashuka Afisa Muunguzi katika Wodi ya Watoto Hospitali ya
Mnazi Mmoja Bi. Fatma Ali Mzee na kushoto Afisa Mfawidhi Msaidizi Bi
Hazina Konde, wakiwa katika moja ya Wodi ya Watoto katika hospitali mpya
ya Watoto Mnazi Mmoja.
Maafisa
Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya
vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya
kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto
Zanzibar.
Maafisa
Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya
vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya
kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto
Zanzibar.
Maafisa
wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitoka katika jengo ya hospitali ya
Watoto Mnazi Mmoja baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi msaada wa
mashuka kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto Hospitali Kuu ya Mnazi
Mmoja Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com.
Email othmanmaulid@gmail.com
Mobile.0777424152
EmoticonEmoticon