MACK D BONANZA &FUN RUN KURINDIMA JUNE 07,2025

May 01, 2025


Na Mwandishi wetu



UONGOZI wa Mac D umetangaza tarehe  ya kufanyika bonanza lake katika awamu ya pili ambapo  litaanza  asubuhi  saa 12:00  kutakuwa na mbio za  kujifurahisha 'Fun Run'  zitakazojulikana kwa jina la  'Mac D  Fun  Run 2025' .

Akizungumza na Waandishi wa Hbari leo tarehe 01 Mei 2025  kwenye Ukumbiwa EB Twenty Five uliopo Mbezi Makonde  Jijini Dar es Salaam Mratibu wa bonanza hilo Denzel Deogratius Rweyunga amesema kuwa  bonanza hilo linalofanyika kwa msimu wa pili litafanyika tarehe 07 Juni 2025 ambapo pia  mbio hizo zitaanza  katika Viwanja vya  Chuo Cha  Taifa Cha Jeshi (National  Defence  CollageNDC) Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

"Washiriki wa  mbio za KM 10 na KM5 wataanza  mbio majira ya saa moja asubuhi  kutoka Chuo Cha NDC  wataelekea  uelekeo wa  kwenda  Ununio  na  watakapofika  katika Uwanja wa mpira  unaofahamika kama Ununio  Playground  karibu na Kanisa la Roman Catholic  watageuza  hapo na kurejea katika uwanmja wa NDC.

Amesema kuwa lengo kuu la mbio hizi  kwa mwaka huu  ni kuunganisha  jamii katika  kuboresha afya na  na kuwa wakakamavu  katika kufanya mazoezi  na kulenga kutokomeza  magonjwa yasiyoambukiza  kufahamiana  na kutengeneza marafiki wapya.

"Tunawaalika watu wote  mtu mmoja mmoja, vikundi  vya wakimbiaji  na taasisi  mbalimbali  kushiriki  pamoja nasi  na baada ya kujisajili mshiriki atapata Tshirt bure na kwa yeyote anayependa kushiriki ajisajili kupitia www.macdbonanza .co.tz, vituo vingine vya usajili ni pamoja na EB Twenty Five Mbezi Makonde, Mac D Wines & Spirits Kunduchi, Zaks Bay Boko Magengeni na Leather Men Mabatini Kijitonyama Dar es Salaam.

"Msimu wa pili wa bonanza letu tutaanza na Fun Run  hizi ni mbio za kujifurahisha  na kuweka miili yetu  katika hali nzuri  ya kiafya  ambapo hakuna mshindi  wala zawadi  yeyote itakayoshindaniwa bali washiriki wote watapatiwa  fulana na namba ya kukimbia  bure  pia Kituo cha ITV kitarusha matangazo hayo mubashara" amesema Rweyunga.

Mratibu huyo ameongeza kwa kusema kuwa baada ya Fun Run  kumalizika jioni kuanzia saa 10  timu mbili ambazo ni Mac D  FC na IPP Media watashuka dimbani  na katika mchuano wa mwaka huu  mshindi ataondoka na Kombe na mechi hii itatangazwa mubashara na kituo cha Radio One.

Wakati huohuo Rweyunga ametoa shukrani kwa wadhamini wa bonanza hilo sambamba na kuwatambulisha katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

"Bonanza la mwaka huu limeandaliwa katika viwango vya juu , tunawashukuru  sana wadhamini wetu  ambao wamejitokeza kutuunga mkono ambao ni ITL, Bonite Bottlers (Kilimanjaro Drinking  Water),Bodi ya Utalii Tanzania  (TTB), Isumba Trans  Limited , Zaks Bay Liquar na Pwani Inland  Clearance and Depot (PICD).

Mwisho.

Share this

Related Posts

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng