Na Oscar Assenga,TANGA
WATANZANIA wametakiwa kuendelea kuenzi na kuulinda Muungano uliopo hapa nchini ambayo ni tunu kubwa ilioachiwa na Waasisi wa Taifa kwa miaka 61 sasa iliyopita ikiwemo kudumisha mshikamano na umoja
Hayo yalisemwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuberi Maulidi wakati katika maadhimisho ya Muungano ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Aprili 26 ambayo mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo‘Muungano wetu ni dhamana heshima na tunu ya Taifa shiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025"
Zuberi alisema kwamba ni vema watanzania kuhakikisha wana dumisha umoja na mshikamano hususani wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi ikiwemo kuwasisitizia wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwa upande wa Urais,Ubunge na Udiwani.
Alisema pia ni vema watanzania waliopewa dhamana ya kusimamia sekta mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwawanatekeleza vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamaia maono ya serikali kawenye miradi ya maendeleo.

“Kauli mbiu ya maadhimisho Muungano wetu ni dhamana heshima na tunu ya taifa shiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kauli mbiu hiyo watanzania tumebarikiwa dhamana ya ya muungano wetu waibebe vizuri dhamana hiyo kwa sababu watanzania wanaheshima kubwa kutokana na muungano huo hivyo heshima hiyo ni vema tuendelee kuidumisha tuilinde na hatimaye kujitokeza kwa wingi kujitokeza kuchagua viongozi wetu kwa amani na utulivu kwa maana ndio njia kushiriki kwenye uchaguzi mkuu’ameongeza

Awali akizungumza Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema kwamba tangu kuasisisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia awamu zote ni mambo mengi ya kimaendeleo yamefanyika hususani kwenye awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Sisi ambao tumeukuta muungano wajibu wetu ni kuutuza , mambo mengi yamefanyika lakini katika awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suuhu Hassan yamefanyika mengi zaidi ikiwemo ucumi kuimarika kinachotakiwa ni kuhakikisha kwamba tunakwenda pamoja tukitanguliza mbele maslahi ya muungano wa nchi hizi mbili tunaomba sana amani iendelee kutwala” alisema Dkt. Buriani.
Naye kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dastan Kitandula amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia sekta mbalimbali ikiwamo Afya ,Elimu, Miundombinu ambapo mkoa huo umenufaika kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati.
“Kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Tanga tunampongeza sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika muda ambao tumekuwa wawakilishi wa wananchi hatukuwahi kuona maendeleo makubwa kama haya ya kipindi cha awamu ya sita anayoiongoza” amesema Kitandula.
Mwisho.,

EmoticonEmoticon