Kulia Bwana Navneft
Meneja katika Kiwanda cha Chemicotex, alieleza jambo kwa wajumbe wa msafara wa
Naibu Waziri Mpina katika ziara ya kushtukiza kiwandani hapo leo.
Naibu Waziri Mpina akitolea Msisitizo adhabu ya uchafuzi wa
mazingira aliyoitoa katika kiwanda cha Chemicotex Jijini Dar esSalaam
alipofanya ziara ya kushtukiza leo.
|
NA EVELYN MKOKOI – DAR
ES SALAAM
Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amekitoza faini ya shilingi Milioni 25, kiwanda
kinachotengeneza biadhaa mbali mbali za matumizi ya manyumbani kama vile mafuta
ya kujipaka mwili na dawa za meno cha chemicotex, mkilichopo Mbeji Jogoo jijini
Dar es Salaam Kwa uchafuzi wa mazingira.
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa baada ya wiki mbili inatokana
na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya mazingira unaofanywa na kiwanda hicho
kilichopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ya kutiririsha maji taka na
maji machafu katika mfereji wa maji ya mvua.
Naibu Waziri Mpina ameshangazwa na uthubutu wa uchafuzi wa
mazingira unaofanywa na kiwanda hicho, pamoja na jitihada za serikali kupitia
Ofisi yake na NEMC za kuthibiti uharibifu wa mazingira kwa kutoa adhabu mbali
mbali kwa waharibifu.
“Ujio wangu katika kiwanda hiki unatokana na malalamiko ya
wananchi ya kututiririshiwa maji machafu katika makazi yao na maeneo ya
biashara, hakuna atakaesalimika kwa kosa
la kutokutunza mazingira na afya za watu, alisistiza Mpina”.
“Mpo Barabarani mnachafua mazingira Hadharani bila haibu,
mmedharau jitihada za serikali hii ya awamu ya tano na kuona kama ni nguvu za
soda, adhabu hii ilipwe kama ilivyo elekezwa hatuta kuwa na uvumilivu kwa
muwekezaji yeyote atakaechafua mazingira. Alisema”.
Kwa Upande wake Mwanasheria kutoka NEMC Bw. Heche Mananche
aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa kiwanda endapo hatakuwa tayari kulipa
faini hiyo anaweza kupelekwa mahakamani.
Wakati Huo Huo, Naibu Waziri Mpina Amezindua Mfereji wa
kutirirsha maji katika kiwanda cha Cement cha wazo, baada ya kujiridhirisha na
utekelezaji wa maagizo yake kiwandani hapo katika moja ya ziara zake mwaka jana,
ambapo ilibainika kuwa kiwanda hicho kimekuwa ni kero kwa wananchi majirani kwa
kutiririsha maji na kusababisha mafuriko hasa katika kipindi cha mvua.
Kwa upande wake mkazi wa eneo la wazo bwana David kahaga
aliupengeza uongozi wa kiwanda hicho kwa ujenzi wa mtaro huo na kusema kuwa
umetatua changamoto katika shule ya msingi jirani na kiwanda hicho ambayo
ilikuwa ikikumbwa na mafuriko mara kwa mara hasa katika kipindi cha mvua,
lakini bado wakazi hao wana hofu na usalama wao baada ya ujenzi wa mtaro
huo na kuwa bado wanakabiliana na
changamoto kubwa ya vumbi itokanayo na uchimbaji wa malighafi za uzalishaji
katika kiwanda hicho.
EmoticonEmoticon