Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amefungua mafunzo ya tatu ya Bespoke kwa Mawakili wa Serikali, yalioandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo yameanza tarehe 15 Julai, 2026 na yatahimishwa tarehe 17 Julai, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) Jijini Arusha.
Mhe. Johari amewasisitiza Mawakili wa Serikali kuhakikisha wanasimamia vyema Utawala wa Sheria katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali ipasavyo kuendelea kuzingatia sheria ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050.
“Nitumie fursa hii kuwakumbusha washiriki wote kuwa, tunapoendelea katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050 ni muhimu kufahamu kuwa, Taifa linahitaji zaidi ya utaalamu wetu wa sheria.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aidha, Mhe. Johari amewakumbusha Mawakili wa Serikali kutambua nafasi yao katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, ambapo ameeleza kuwa utekelezaji wa malengo ya yake unategema kwa kiwango kikubwa uwezo wa Mawakili wa Serikali, pamoja na kuwa na mifumo ya kisheria itakayokwenda sambamba na kasi ya maendeleo na mabadiliko yanayoendelea nchini na duniani kote.
“Ni imani yetu kuwa, Dira hii itatekelezwa kwa kiwango kilichokusudiwa kwa kupitia Sheria bora, Sera madhubuti, Mikataba yenye tija, Mifumo bora ya utawala wa kisheria sambamba na taasisi zenye uwezo wa kutafsiri malengo ya maendeleo kuwa matokeo yanayoonekana kwa manufaa ya Taifa lote kwa ujumla.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewahimiza Mawakili wa Serikali kuzingatia matumizi ya teknolojia ambayo yamebadilisha kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma za kisheria ikiwemo matumizi ya Akili Mnemba na utoaji wa matumizi ya Ushahidi wa Kielektroniki.
*“Mapinduzi ya teknolojia yamebadilisha kwa kiasi kikubwa, namna ambavyo huduma za kisheria zinaendelea kutolewa nchini na duniani kote kwa ujumla, hivyo katika mazingira haya, Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria hawawezi kuendelea kutekeleza majukumu yao.














EmoticonEmoticon