Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu ya Tigo kuja na vifurushi vipya vya intaneti ;Mega Mix'. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
|
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza
kuanzishwa kwa ofa ya MEGA MIX ambayo itakuwa inatoa vifurushi vya
intaneti ambayo vitawazawadia wateja dakika za ziada kwa ajili ya kupiga simu.
Ofa hii itawapatia wateja urahisi wa kutumia vifurushi hivi
vipya kupitia kifaa chochote kinachotumia intaneti zikiwemo simu za
mkononi na modemu.
Akitangaza vifurushi vya
Mega Mix kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev
alivielezea vifurushi hivyo kama “hatua moja mbele ya mabadiliko katika
soko inayotoa vifurushi sahihi zaidi: ikiwa ni suluhisho kwa
watumiaji wote wa data ndani ya sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania.”
Shavkat
aliongeza, “Wateja wetu hivi sasa wana uhuru wa kuchagua
kutoka katika simu zao kifurushi chochote wanachokitaka kikiwa na
dakika za ziada zitakazo wawezesha kuunganishwa na wapendwa wao
wakati tunapoukaribisha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.”
Aliendelea kusema,
“Kwa vifurushi vipya wateja wanaweza kuhabarishwa kwa wakati katika mtiririko
wa kuunganishwa na wenzi wao na kuwa bega kwa bega na
yanayotokea sehemu mbalimbali duniani. Vifurushi hivi vipya vinaendelea
kuonesha jinsi Tigo ilivyojikita katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa
maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa
pamoja na ubunifu kwa wateja wetu.
“Wateja wetu vilevile
wanaweza kuzipata taarifa za kidunia, kutafuta kupitia Google, kusikiliza
muziki, kuangalia video, kupakua na hata kutiririsha sinema. Hii ni kwa
sababu tumeunda vifurushi hivi kwa kuzingatia mahitaji ya kipekee
ya wateja wetu kwa kufanya uwepo urahisi katika kuchagua
kutoka katika kifurushi kimoja kwenda kingine kutegemeana na
hali ya kifedha ya wateja.”
Aidha Meneja Chapa wa
Tigo, William Mpinga alisema, “Kutokana na teknolojia ya 4G LTE kupatikana
kwa hivi sasa katika miji 20 vifurushi vya Mega Mix
kunafungua enzi mpya za kufikia intaneti kusiko na ushindani, ambako
kutaondoa vikwazo na kuwawezesha watumiaji kuona mengi, kusikia
zaidi na hatimaye kupata yaliyo mazuri katika maisha.”
Mpinga aliongeza, “Mteja
anachotakiwa kukifanya ili kupata vifurushi vya Mega Mix ni kupiga
*148*00# halafu chagua, ‘Vifurushi vya intaneti.”
|
Share this
EmoticonEmoticon