BANDA LA MAONESHO LA TANZANIA LANG'ARA KWENYE MKUTANO WA TICAD VI

August 28, 2016


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka mara baada ya kuwasili kwenye Banda la Maonesho la Tanzania yanayofanyika wakati wa Mkutano wa TICAD VI Jijini, Nairobi. Makampuni na Taasisi mbalimbali kutoka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na Japan yanashiriki maonesho hayo yanayolenga kuvutia wawekezaji na wafanyabishara. 
Mhe. Naibu Waziri akipata maelezo kuhusu bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Tanzania zilizokuwepo kwenye Banda hilo. Bidhaa hizo ni pamoja na Kahawa, Majani ya Chai na Viungo vya chakula.
Banda la Tanzania kama linavyoonekana.
Mhe. Waziri akipata maelezo ya namna watu wa makampuni mbalimbali walivyovutiwa na kahawa ya Tanzania.
Mhe. Naibu Waziri akikaribishwa na Bi. Latifa Kigoda, Afisa Mwandamizi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) alipotembelea banda la Tanzania.
Mhe. Naibu Waziri akisaini kitabu cha wageni bandani hapo.
Mhe. Naibu Waziri akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Kigoda kuhusu namna TIC ilivyojipanga kutangaza fursa za uwekezaji kwa wawekezaji mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa TICAD VI.
Bi. Kigoda akimpatia Jarida Maalum lililoandaliwa na TIC kwa ajili ya kuvutia wawekezaji waliohudhuria mkutano wa TICAD VI.
Bi. Kigoda akimpatia maelezo Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Waziri ambaye alikuwa amefuatana na Mhe. Naibu Waziri.
Mmoja wa wageni aliyetembelea bandani hapo akipata maelezo ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini kutoka kwa Bi. Kigoda.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Susan Kolimba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Lameck Borega, Meneja wa Uwekezaji wa EPZA. 
Mhe. Dkt. Kolimba akimpatia ushauri wa namna ya kuwashawishi wawekezaji kuja nchini kuwekeza kupitia EPZA.
Mhe. Naibu Waziri akiwa amewasili kwenye Banda la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kupatiwa maelezo na Bi. Alistidia Karaze, Afisa Utafiti Mkuu kwenye Bodi hiyo.
Mhe. Naibu Waziri akimpatia ushauri Bi. Karaze wa namna ya kuboresha huduma za utalii nchini ikiwemo maonesho ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »