KIWANDA CHA TWIGA CEMENT CHA WAZO CHAPEWA MWEZI MMOJA KUREKEBISHA MFUMO WA UTOAJI TAKA ILI KUNUSURU MAZINGIRA.

July 12, 2016

              
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Uongozi wa kiwanda cha twiga cement,pamoja na Maafisa kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira(NEMC)alipofanya ziara mapema hii leo.           



Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,luhaga Mpina (katikati)na Meneja mazingira kiwandani hapo bw. Richard Magoda akitembezwa ndani ya kiwanda  baada ya kupata malalamiko ya uchafuzi wa mazingira  kutoka kwa wananchi.          

Baadhi ya Sehemu za Uzalishaji ndani kiwanda hicho ambayo yanalalamikiwa na Wanachi kwa Uzalishji vumbi linalowaathiri wananchi.
EVELYN MKOKOI DAR ES SALAAM

Kiwanda cha kutengeneza cement cha Twiga cement cha wazo jijini Dar  Es Saalaam kimepewa muda wa mwezi mmoja kurekebisha mfumo wao wa utoaji taka ili kunusuru uharibifu wa mazingira na maisha viumbe hai.

Hayo yamesemwa Leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho.

Mhe. Mpina amekitaka kiwanda hicho  kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupima vumbi litokanalo na uzalishaji kiwandani.. ili kuona kama ni la kiwango ambacho si hatarishi kwa mazingira na viumbe hai vinavyozunguka maeneo hayo.

Maagizo hayo ya Naibu waziri Mpina yametokana na malalamiko ya wananchi wa maeneo jirani na kiwanda hicho yanayoeleza kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wakazi au majirani wa maeneo hayo.

Aidha amemtaka muwekezaji huyo kuimarisha mahusiano baina ya kiwanda hicho na wananchi na kufanyia marekebisho kasoro zilizoonekana kujitokeza kiwandani hapo na kuwaasa wawekezaji wa kiwanda hicho kufanya kazi pamoja na kuheshimu sheria hususan za mazingira.

Kwa upande wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira Nemc kumeonekana kuwa na uzembe katika ufuatiliazi wa utekelezaji wa sheria za mazingira hasa kiwandani hapo, baada ya mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa baraza hilo Bi Ruth Lugwisha kushindwa kujibu swali aliloulizwa na Naibu waziri Mpina kuwa ni lini Mara ya mwisho baraza hilo lilijiridhisha kwa kuchukua vumbi kiwandani hapo na kulipima ili kujua lina athari kwa kiasi gani kwa mazingira na viumbe hai.

Kwa upande wake Meneja wa Mazingira wa kiwanda hicho Bw. Bw. Richard Magoda amejitetea kuwa kiwanda kina mahusiano mazuri na wanachi kwani kimeweza kutoa misaada katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na vyandarua na kuchonga barabara za baadhi ya mitaa.

Wakati huo huo viongozi wa serikali za  mitaa Bw. Gration Mbelwa ambaye ni mwenyekiti wa kata ya madale na  Atilio Maginga mwenyetiki wa serikali ya mtaa wa mivumoni..wametofatofautiana kwa  kusema kwamba kiwanda kina mashirikiano mazuri na wananchi, wakati mwenyekiti wa kata ya madale akiwakilisha wanachi kwa kulalamika kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wananchi..

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »