Afisa
Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard
akizungumza na wananchi wa Ukonga pamoja na maeneo mengine ya mji wa Dar
es Salaam kuhusu Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa Semina ya
Ujasiriamali Ukonga jana jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard
akifafanua jambo kwa wajasiriamali kuhusu Mfuko wa Hiari wa PSPF jana
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mjasiriamali kwanza
Enterprises Dr. Didas Lunyungu.
Wajasiriamali
kutoka maeneo ya Ukonga na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam
wakisikiliza kwa makini elimu iliyokuwa ikitolewa kuhusu uchangiaji wa
hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa semina ya wajasiriamali
jana jijini Dar es Salaam
Afisa
Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe akitoa elimu
kwa wachangiaji wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa
kuandikisha wachangiaji wapya wa mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa
Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe akitoa elimu
kwa wachangiaji wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa
kuandikisha wachangiaji wapya wa mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa
kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Mrisho Ngongo (kulia) akitoa fomu
za kujisajiri kwa wachangiaji wapya wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa
PSPF jana jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya wanachama wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakiwa katika
mstari kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho za kujisajiri katika
mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa
Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe (kushoto)
akikagua fomu za uanachama wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF baada
ya kusajili wanachama wapya jana jijini Dar es Salaam.Picha na: Genofeva
Matemu – Maelezo
…………………………..
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Wananchi
zaidi ya 500 kutoka zoni ya ukonga jijini Dar es Salaam wamejitokeza na
kujisajiri kuwa wanachama wa hiari katika mfuko wa hiari wa PSPF ili
kuweza kunufaika na mafao yatolewayo na mfuko huo.
Wananchi
hao walipata fursa ya kujisajiri wakati wa semina ya ujasiriamali
iliyofanyika siku ya jana maeneo ya Ukonga jijini Dar es Salaam na
kuudhuriwa na wananchi wapatao 1600 kutoka zoni ya Ukonga na maeneo
mengine ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Akizungumza
wakati wa semina hiyo Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Delphin Richard amesema kuwa mfuko wa hiari
wa PSPF uliundwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuwa na akiba ya
ziada kwa kutoa uhuru kwa mwanachama kuchangia kwa kutegemea
upatikanaji wa kipato cha ziada kitakachomwezesha kujiwekea akiba.
Bw.
Richard amesema kuwa lengo la PSPF ni kushiriki katika masuala
mbalimbali ya kijamii ili kuweza kutoa elimu ya mfuko wa hiari wa PSPF
hivyo kutoa nafasi kwa wajasiriamali, wakulima, wafugaji,
wafanyabiashara, na watu binafsi kuchangia katika mfuko wa hiari kipato
chao cha ziada kwa ajili ya akiba ya ziada.
Kwa
upande wake Afisa Masoko Bibi. Sarah Adebe amesema kuwa jamii imekua na
muitikio mkubwa wa kujisajiri katika mfuko wa hiari wa PSPF kwani mfuko
huo unatoa huduma kwa kuchangia gharama ndogo hivyo kuwanufaisha
wanachama hasa wa kipato cha chini.
Naye
Mjasiriamali kutoka zoni ya Ukonga Bi. Doris Kimaro amesema kuwa ujio wa
elimu ya mfuko wa hiari wa PSPF ni mafanikio makubwa katika familia
yake kwani atatumia nafasi aliyoipata kwa kuchangia kipato chake cha
ziada ili aweze kunufaika na fao la elimu litakalomuwezesha kukidhi
mahitaji yake ya baadae.
Mfuko
wa hiari wa PSPF umelenga kusaidia jamii kwa kuwa na mafao saba ambayo
ni fao la elimu, fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kifo, fao la
ugonjwa/ulemavu, fao la kujitoa na fao la matibabu.