Mwenyekiti
mpya wa ccm mkoa wa Arusha Maiko Lekule aliyepata kura 515akizungumza
mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho hivi karibuni jijini
Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Katibu
mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Arusha Shabani Mdoe aliyeshinda na fasi
hiyo kwa kupata kura 36 ambaye kwa taaluma ni mwandishi wa habari akitoa
neno la shukurani kwa wajumbe wa mkutano huo mara baadaa ya kutangazwa
rasmi kushinda nafasi hiyo
Msimamizi
wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa Stephen
Wassiraakitangaza rasmi nafasi ya mwenyekiti wa mkoa ambapo pia
aliwataka wanaccm kuhakikisha wanashirikiana
Mjumbe
wa NEC taifa toka wilaya ya Monduli Namelock Sokoine akizungumza katika
mkutano huo mara baada ya uchaguzi kuisha ambapo aliwataka wanaccm
kuchapa kazi na kuhakikisha wanawashuhulikia mamluki waliopo ndani ya
chama hicho
Mjumbe
wa NEC taifa toka wilaya ya Monduli Namelock Sokoineakiteta jambo na
Mbunge viti maalum Catherine Magige katika mkutano huo
Emanuel
Makongoro ambaye alikuwa akiwania nafasi wa uwenyekiti wa mkoa
akifurahia jambo na katibu wa wazazi mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau
Semi
Kiondo ambaye alikuwa akiwania nafasi ya ukatibu mwenezi akizungumza
mara baada ya uchaguzi kuisha ambapo alihaidi kutoa ushirikiano wake kwa
chama cha mapinduzi huku akishirikiana na viongozi waliochaguliwa
viongozi wa chama cha mapinduzi wakiwa katika pozi la picha
Wajumbe wa mkutano
CHAMA cha Mapinduzi (
CCM)mkoa wa arusha kimefanya uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa na
kufanikiwa kumchagua Maiko Lekule aliyepata kura 515 dhidi ya mgombea
mwenza Emanuel Makongoro aliyepata kura 338,huku katibu mwenezi wa chama
hicho akichaguliwa kuwa ni Shabani Mdoe aliyeshinda na fasi hiyo kwa
kupata kura 36.
Aidha katika uchaguzi huo
wa mwenyekiti wajumbe halisi waliopaswa kuhudhuria ni 960 ambapo
waliohudhuria ni 903 huku wajumbe halisi waliopiga kura wakiwa ni 861.
Akitangaza matokeo hayo
jana msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm
taifa Stephen Wassira alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa huru na
amani na hivyo ana imani kuwa uongozi huo utakiletea mabadiliko makubwa
chama cha mapindizi katika mkoa huo.
Alisema kuwa katika mkoa wa
arusha matatizo ya umoja na tofauti yapo na kwamba atakayemaliza mzizi
huo ni mwenyekiti aliyepatikana kwa kuhakikisha kuwa anawaunganisha
wana ccm ili wawe kitu kimoja.
“hapa arusha yapo matatizo
sana naomba tu nitumie fursa hii kumtaka mwenyekiti aliyeshinda
kuhakikisha kuwa anakijenga chama na ndie atakayeifanya arusha iungwe
mkono na watu wote hatutaki kusikia tena kuwepo kwa makundi ya kuvunja
chama muda wa uongozi wa mwaka mmoja ni mkubwa sana katika kukirejesha
chama sehemu yake”alisema Wassira.
Alileleza kuwa kwa arusha
hawataki kusikia ccm inayoendeshwa kwa fedha ya mtu binafsi wala
kampuni bali wanaitka ccm yao irudishe kwa wananchi na jamii iweze
kunufaika na rasilimali zake sio kwa ajili ya watu binafs ambao ndio
wamekuwa wakikisaliti chama.
Kwa upande wake mwenyekiti
aliyechaguliwa Maiko Lekule akitoa neno la shukrani alisema kuwa
anawashukuru wajumbe hao kwa kumchagua na kwamba nafasi aliyopewa
hataweza mwenyewe kuimaraisha chama hicho ambacho kipo mahututi hivyo
anaomba ushirikiano uwepo.
Lekule alisema kuwa chama
hicho kinahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa sana hivo kamati za siasa
,wenyeviti na kamati inabidi waungane kwa pamoja kukijenga chama hicho
kwa upya ili kirudi katia hali yake.
“mimi nahidi tu
ntakiimarisha chama hiki kwa kushirikiana na wenzangu ila niwaombe tu
mamluki wote walioko kwenye hiki chama ambao ndio wasaliti wakuu
waondoke mapema wenyewe na kama hawataondoka tutawaondoa sisi”alisema
Lekule.
Nae
katibu mwenezi Shabani mdoe ambaye ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la
Uhuru aliwashukuru wajumbe hao kwa kumuamini kwa kumchagua na kuahidi
kuwa atatumia taaluma yake ya uhabari kuimarisha chama hicho kwani
waandishi wana nguvu kubwa ya kujenga palipobomoka.