Na Jamiimojablog
Ujuzi,
katika soko la ajira ni mali ambayo inahitaji matengenezo na uboreshaji. Kama
mali nyingine yoyote, matumizi yake bora, hukuzalishia zaidi. Sababu nyingi zimetolewa
katika kipindi cha miaka mingi kwamba kuna utofauti wa wazi baina ya mtu mwenye
elimu aliyeko kazini na mwenye elimu bila kazi. Utofauti huo ni jinsi ujuzi wa
watu hao wawili unavyotumika.
Vijana
wengi wa Tanzania wana ujuzi waliopata kutokana na mafunzo mbalimbali, lakini
baadhi yao kushindwa kutumia ujuzi walionao. Sababu pekee inayosababisha hili
ni; mahitaji ya ujuzi katika soko la ajira hayako sambamba na ujuzi utolewao.
Matokeo yake ni vijana kujikuta kwenye sintofahamu iliyosababishwa na mgongano
wa kiujuzi. Ushindani mkubwa katika soko la ajira duniani ni kuongezeka kwa
matumizi ya TEHAMA ambayo imechukua nafasi kubwa ya ajira za watu, na kama
ajira inahitajika basi mtu ni lazima uwe na ujuzi maalumu.
Mwalimu
mjini Arusha mwenye ujuzi wa TEHAMA ana nafasi kubwa ya kupata ajira kuliko yule
asiye na ujuzi huo. Karani jijini Dar es Salaam mwenye ujuzi wa teknolojia ya
juu ana nafasi kubwa ya ajira kuliko yule asiye na ujuzi huo. Tour guide mkoani
Morogoro mwenye ujuzi wa mitandao ya kijamii na ulimwengu wa kidijitali ana uwezekano
mkubwa wa kugundua fursa mpya kuliko yule asiye na ujuzi huo. Mwana masoko wa
Mbeya mwenye maarifa zaidi juu ya matumizi ya mitandao ana nafasi kubwa ya
kuvutia watu zaidi ya yule anayeendelea kutegemea mbinu za kizamani. Orodha ni
ndefu.
Umewahi
kujiuliza kwa nini Ronaldo, Messi, Rooney, Usain Bolt, Venus, Serena na wanamichezo
wengine wameendela kutamba katika tasnia ya michezo kwa muda mrefu? Siri imelala
katika kuboresha ujuzi wao. Ili umuhimu wa mtu uonekane katika soko la ajira, lazima uwe na ujuzi husika na
uendelee kuuongeza mara kwa mara.
EmoticonEmoticon