Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima
akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza
la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano
wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza
ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza la Usalama
Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Katikati ni Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini Malawi ambaye pia ni Kiongozi wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini humo, Maepheson Matowe. Mkutano
huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa
Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa
makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani)
katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya
jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda
sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo . Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mtoa mada wa Mkutano Mkuu wa
Wadau wa Usalama Barabarani ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof.
Samweli Manyele akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote
nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali
ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Prof. Manyele alitoa
elimu ya jinsi ya kusafirisha salama kemikali. Mkutano huo ambao unaenda
sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame
Silima (katikati meza kuu) akijadili jambo na Kamanda wa Kikosi cha
Polisi
EmoticonEmoticon