harambee wa ujenzi wa Kanisa la KKKT mkoani Rukwa – yafana

July 20, 2015

1
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijadiliana jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (katikati) na Askofu Ambele Mwaipopo wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, wakati wa harambee wa ujenzi wa Kanisa la KKKT mkoani Rukwa. Katika harambee hiyo Nyalandu, aliyekuwa mgeni rasmi alichangia sh. Milioni 100. Harambee hiyo ilifanyika jana usiku katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
2 3
ASKOFU Ambele Mwaipopo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, akimkabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na waumini wa kanisa hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati wa harambee ya kuchangia kanisa.
4
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akimkabidhi zawadi maalumu aliyopewa na Papa Francis XIV, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wa sh. Milioni 100 alioutoa kuchangia ujenzi wa kanisa mjini Sumbawanga.
8
5
WAUMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), waliohudhuria harambee hiyo wakishangilia kwa furaha baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kutangaza kuchangia sh. Milioni 100 kusaidia ujenzi wa kanisa jipya la KKKT mjini Sumbawanga.
6
9
7
BAADHI ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), waliohudhuria harambee hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Waziri wa Maliasi na Utalii, Lazaro Nyalandu (hayupo pichani), wakati akihutubia.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »