Afisa Mwandamizi katika sekta ya benki, Dkt. Danford Muyango ametangaza kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Urambo mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na BMG Media, Dkt. Muyango amesema Urambo inamhitaji ili akashughulikie changamoto za wana Urambo ikiwemo uhaba wa masoko ya mazao ya biashara ikiwemo Tumbaku, kukuza sekta ya viwanda, upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na miundombinu bora ya barabara.
Dkt. Danford Muyango anatarajiwa kuchuana na wagombea mbalimbali akiwemo mbunge anayemaliza muda wake, Mama Margaret Sitta.
Dkt. Muyango amesema "Urambo inahitaji mtu anayeijua na mwenye uwezo wa kutatua changamoto nne ambazo ni masoko ya zao la Tumbaku na mazao mengine ya niashara, kukuza viwanda wa mazao ya chakula na uongezaji thamani. Majisafi na salama kwa ngazi ya Mitaa na miundombinu inayofikika. Nimeyaishi maisha haya na nipo tayari kutatua changamoto hizi chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM)".
Ifahamike kuwa Dkt. Muyango ni mbobevu wa mambo ya fedha na maendeleo kwa mgazi ya udaktari (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Alizaliwa katika Kijiji cha Usoke Mission, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora ambapo pia alipata elimu ya msingi na Sekondari miaka ya 1990.
Muyango ni Afisa Awandamizi katika masuala ya benki ambapo amehudumu kwa zaidi ya miaka 18 katika mabenki mbalimbali.
Kazi na Utu: Tuikomboe Urambo
EmoticonEmoticon