Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda ameendelea kuungwa mkono na
wajumbe wa Mkutano wa 36 ambao ni Maspika na Wabunge kutoka Umoja wa
Chama cha Mabunge ambao ni wanachama wa nchi za kusini wa Jangwa la
Sahara (SADC PF) kugombea nafasi ya Urais ya Umoja huo ili aweze
kuongoza kwa kipindi cha miaka 2 ijayo katika chama hicho.
Jitihada
hizo zimeendelea kujitokeza hapa Victoria Falls ambako mkutano huo
unafanyika baada ya baadhi ya Maspika wa Nchi za SADC pamoja na wabunge
wao kuomba miada ya kukutana naye na kumwambia dhahiri kuwa nchi zao
wanamuunga mkono na wangependa aweze kushiriki uchaguzi huo ili waweze
kumchagua awaongoze katika kipindi cha miaka miwili kutimiza malengo
waliyojiwekea katika umoja huo.
Mkutano
huo wa 36 wa Wabunge wa SADC umeanza tangu tarehe 26 Oktoba 2014 hapa
mjini Victoria Falls nchini Zimbabwe na unatarajiwa kumalizika tarehe 3
Novemba, 2014, na mojawapo ya agenda za mkutano huo ni uchaguzi wa rais
wa chama hicho baada ya rais anaemaliza muda wake ambaye pia ni Spika wa
Mauritius Mhe. Abdool Razack Mahomed Ameen Peeroo,kutakiwa kukabidhi madaraka kwa rais Mwingine atakayepatikana katika Mkutano huu baada ya kipindi chake kumalizika.
Uchaguzi
wa rais wa Umoja huu wa mabunge ya SADC utafanyika tarehe 2 Novemba,
2014, ambapo kwa kuwa nafasi hii ni ya mzunguko kwa nchi za ukanda huu,
kwa mzunguko uliopo hivi sasa nchi zinazopewa nafasi ya kuleta mgombea
ni tatu ambazo ni Tanzania, Msumbuji, na Seychelles ambapo kila Spika
kutoka nchi hizi atapigiwa kura ili aweze kupatikana mmoja wapo
atakayeongoza Umoja huu kwa miaka miwili ijayo.
Licha
ya kwamba wagombea ni watatu, tayari wajumbe wamkutano kutoka nchi
mbalimbali za SADC wamekuwa wakifanya jitihada za Makusudi ili Spika
Makinda aweze kupewa nafasi hii waweze kutumiza malengo waliyokuwa
mamejiwekea.
Akizungumza
na Mhe. Makinda mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Bunge hilo la SADC Mhe.
Sylvianne Valmont kutoka Ushelisheli amesema “tunajua kuwa wewe sio
kwamba ni mgeni katika Umoja huu, ushawishi unaojitokeza kutoka kwetu
unataokana na mafanikio makubwa uliyoyaleta katika chama hiki pindi
ulipokuwa Makamu wa rais wa Umoja huu mwaka 2008 hadi 2010”
Akielezea
zaidi baadhi ya mafanikio ya uongozi wake akiwa Makamu wa rais Mhe.
Valmont anasema ni jitiohada za makusudi za kuongoza ujumbe wa Wabunge
wanawake kutoka nchi za SADC kwenda katika nchi za Botswana, Malawi,
Mozambique na Zambia kwa lengo la kuwashaiwshi viongozi wa Mataifa hayo
kuongeza idadi ya uwakilishi wa wanawake katika mabunge yao angalau kwa
asilimia 30, zoezi ambalo lilifanikiwa sana.
Nae
Mjumbe kutoka Swaziland Mhe. Sikhumbazo Ndlovu anasema Mhe. Makinda
anaweza kuongoza umoja huu na kuupeleka kwenye mafanikio zaidi kutokana
na ushawishi Mkubwa iliyonayo Nchi ya Tanzania katika nchi wanachama wa
SADC swala ambalo linafanya wajumbe wengi wa Umoja huu kuamini kuwa
chini ya uongozi wake atasaidia sana kusukumu baadhi ya maswala ya chama
hiki kwa Serikali za nchi wanachama.
Kwa
upande wake Makinda amewahakikishia Wajumbe wa Mkutano huo kuwa
atahakikisha anatimiza matarajio ya wanachama wa umoja huu hususani
kuufanya umoja huu kuwa bunge madhubuti la SADC cha msingi ni
kuhakikisha wanampigia kura kama wanavyo ahidi.
Pamoja
na hilo Mhe. Makinda anasema kukubalika kwa Tanzania katika Ukanda huu
wa SADC na kampeni inayofanywa ili aweze kuongoza Bunge hili la SADC
unatokana na historia Tanzania iliyojiwekea tangu wakati wa Ukombozi wa
Bara la Afrika mwanzoni mwa miaka ya 1960, ambapo Tanzania chini ya
Uongozi wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, nchi
yetu ilijitwalia heshima mbele ya uso wa kimataifa kutokana na mchango
wake wa kulikomboa bara la Afrika kutoka katika uongozi wa kikoloni hususan katika Kutoa mchango wa ukombozi kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrikakama vile, Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC),Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).
Uchaguzi
wa Rais wa chama hiki mwaka huu, unakuja kukiwa na matarajio makubwa ya
kuanzishwa kwa Bunge madhubuti la SADC ambapo Katibu Mkuu wa umoja huu
Dk Esau Chiviya, anasema kauli mbiu ya mwaka huu ambayo inasema “Bunge
la kikanda la SADC – Wakati ni huu” inazingatia na kuhitimisha matarajio
ya waasisi wa umoja huu ya kuwa na Bunge imara la ukanda huu wa SADC
ambapo anaamini kuchaguliwa kwa rais wa umoja huo lazima kwende sambamba
na uwezo wake kuweza kufanikisha jambo hili haraka iwezekanavyo.
“
Tunaaamini rais tutakayempata katika mkutano huu unaweza kuharakisha
kuweza kushirikiana na wakuu wanchi za SADC kuweza kufanya umoja huu
kuwa Bunge kamili la SADC na lenye nguvu kimaamuzi” anasema Dkt. Chiviya
Kwa
hivi sasa Rais Robert Mugabe ndiye mwenyekiti wa wakuu wa nchi za SAD
ambapo endapo spika Makinda atachaguliwa kuwa rais wa chama hiki
atasaidia kuendelea kumshawishi Rais Mugabe ili suala la kuanzishwa kwa
Bunge hilo la ukanda wa SADC linakuwa moja ya agenda kuu katika Mkutano
ujao wa wakuu wa Nchi za SADC unaotarajiwa kufanyika Mwakani 2015 nchini
Botswana.
Katika
mkutano huo wa mwaka wa umoja wa Mabunge ya SADC Mhe. Makinda anaongoza
ujumbe wa Wabunge sita kutoka Tanzania ambao ni Mhe. Seleman Jafo, Mhe.
Anna Abdalah, Mhe. Mohamed Mnyaa, Mhe. Goodluck Ole-Medee, na Mhe.
Stella Manyanya.
Zaidi ya Wabunge 100 ikiwa ni pamoja na Maspika wa Mabunge ya nchi za SADC wanashiriki Mkutano huu.
EmoticonEmoticon