Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja
wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo mara baada ya kuwasili akitokea
katika ziara yake ya Ulaya na Mashariki ya Kati Oman.
Baadhi ya viongozi alioongozana nao katika ziara hiyo wakiwa katika mkutano huo.
…………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imeanza kulifanyia kazi
tatizo la wakulima kukosa mahali pa kuhifadhia ya mazao yao, hivyo
litapatiwa ufumbuzi katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo
baada ya mpango wa kujenga maghala makubwa kuanza.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda katika mkutano wake na
waandishi wa habari alioufanya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K.Nyerere uliopo jijini Dares
Salaam kufuatia ya ziara yake ya kikazi katika nchi za Uingereza, Poland
na Oman. yenye lengo la kuhimarisha mahusiano.
Waziri Mkuu Pinda alisema ametembelea nchi ya Poland, ambayo ilikuwa na
lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano na kutafuta msaada wa
mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu wa kusaidia kupambana na tatizo la
uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia nafaka au chakula.
Alisema katika nchi hiyo amejionea jinsi ilivyo kuwa na mfumo maalum wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chakula.
“Unahitajika mfumo huu wa Poland wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi
chakula. Hivyo tunahitaji kiasi cha fedha cha Sh. bilioni 240 hadi
bilioni 260 kwa ajili ya kukabilian na tatizo hili, tumeandika ombi na
tumeshapeleka kwa Serikali,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Aliongeza kwamba pia wameomba mkopo wenye masharti nafuu ili kusaidia
kupambana na tatizo la uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia chakula,
hivyo kwa kuanzia wameomba mkopo wa Euro milioni 500 katika nchi ya
Poland,ambao wenye riba nafuu ya kiasi cha 0.25.
Alisema lengo ni kujenga maghala kubwa katika baadhi ya mikoa, ambayo
aliitaja kuwa ni Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Dodoma, Tanga na ghala
dogo katika Kanda ya Ziwa.
Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mahindi nchini alisema wakulima
wameweza kuzalisha tani 500,000 za mahindi, lakini changamoto iliyopo
iliyopo ni mahali pa kuhifadhia.
Aliongeza kuwa uwezo wa maghala ya Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa
Chakula(NFRA) ni tani 240,000 wakati bado kuna tani zaidi ya 200,000
zilizozalishwa mwaka jana (msimu uliopita) za mahindi na katika kipindi
cha sasa wamepanga kununua tani 3.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali imeshirkisha sekta binafsi ili iweze
kununua tani 200,000 na lakini bado chakula ni kipo cha kutosha.
Alisema kwa upande wa mpunga kuna tani zaida 800,000 kwani msimu huu
zilimezalishwa tani milioni 1.5. hali hiyo imechangiwa na matumizi ya
mbegu bora, mbolea na matumizi ya matrekta.
Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa juhudi zao za kulizalisha chukula cha kutosha.
Akizungumzia kuhusu ziara yake nchini Oman alisema ilikuwa na lengo la
kuhimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.
Alisema nchi hiyo mwikitio wa nchi hiyo wa kuwekeza ni mzuri hususan kwenye kilimo, mifugo na uvuvi.
“ Eneo walioonesha hisia ni la mifugo, hasa
EmoticonEmoticon