“RC GALLAWA AAMURU MKAGUZI WA NDANI WA HALMASHAURI AWEKWE NDANI”

October 30, 2014





MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu ChikU Gallawa amemuagiza Mkuu wa
Jeshi la Polisi wilaya ya Tanga(OCD)Omari Ntungu kumkamata Mkaguzi wa
ndani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Hassani Njama na kumuweka ndani
mpaka atakapomaliza ziara yake kwa kushindwa kuwepo eneo la usimamizi
wa mradi wa ujenzi wa maabara.



Agizo hilo la Gallawa alilitoa  juzi wakati alipofanya ziara ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara kwenye shule mbalimbali
zilizopo wilaya ya Tanga Tanga ambapo akiwa kwenye shule ya sekondari
Toledo iliyopo Kata ya Mwanzange jijini ndio alipobaini mkaguzi huyo
kutokuwepo eneo lake la kazi wakati ujenzi ukiendelea.

Akiwa shuleni hapo Mkuu huyo wa mkoa alibaini kuwepo kwa ujenzi
usioridhisha na kutaka maelezo kutoka kwa mkaguzi wa ndani kuhusu hali
hiyo ambapo alibainika kutokuwepo jambo ambalo lilimshangaza sana na
kulazimika kuchukua uamuzi huo.

Alisema kuwa kimsingi maelezo mengi kuhusu ujenzi huu wa maabara
yalipaswa kutolewa na mkaguzi huo hivyo kutokuwepo kwake kunaonyesha
kitendo cha kushindwa kuwajibika ipasavyo kwenye eneo lake la kazi
hivyo lazima achukuliwe hatua.

    “OCD nasema mkamate mkaguzi huyu wa Halmashauri mpaka ziara yangu
itakapomaliza hii sio sahihi ujenzi wa maabara unaendelea nay eye
kushindwa kuwepo eneo la mradi huu hii sio sawa kwa sababu unaweza
kujengwa chini ya kiwango kutokana na kutokuwepo usimamizi mzuri

Shule ya sekondari ya Toledo ni miongoni mwa shule za sekondari za
kata ambazo zimepangwa kupandishwa kwa  kuanzishwa kidato cha tano na
sita ili kuweza kuchukua wanafunzi wanaofaulu kwenye shule za
sekondari za kata jijini Tanga.

Katika hatua nyengine,RC Gallawa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Jiji la Tanga,Juliana Malange kuwasimamishia mishahara yao Afis
Mtendaji wa Kata ya Chumbageni Zuhura Shehe na watendaji kumi na moja
wa mitaa kwenye Kata hiyo mpaka ujenzi wa maabara katika shule ya
sekondari utakapomalika.

Alisema kuwa kimsingi hilo linatokana na watendaji hao kuzembea
kusimamia na kuhimiza ujenzi wa maabara hizo kwenye maeneo yao kwa
kushindwa kuweka mipango mizuri ya ukusanyaji wa michango ambayo
ingewezesha kukamilika kwa ujenzi huo.

   “Mimi nadhani hawa watendaji kwenye mitaa ambao wameshindwa
kusimamia ujenzi wa maabara kwenye maeneo yenu msimamishiwe mishahara
yenu mpaka pale ujenzi huo utakapokamilika kwa sababu jambo mmeshindwa
kusimamia suala hili “Alisema Gallawa.

Hata hivyo alisema kuwa licha ya kusimamishwa kwa mishahara hiyo
lakini watendaji hao wachukuliwe hatua za kinidhamu na mamlaka husika
kutokana na kushindwa kusimamia miradi ya ujenzi huo kwa wakati
ulipopangwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »