RCL YAANZA KUTIMUA VUMBI KATIKA VITUO VITATU
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
inayoshirikisha timu 27 inaanza kutimua vumbi kesho (Mei 10 mwaka huu) katika
vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku.
Kundi A
ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, African Sports
ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8 mchana wakati saa 10
jioni ni Mji Mkuu FC (CDA) ya Dodoma dhidi ya Pachoto Shooting Stars ya Mtwara.
Jumapili
(Mei 11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Bulyanhulu FC
(Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8 mchana wakati saa 10 jioni
ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia ya Dar es Salaam.
Kundi B
katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya litaanza ligi kwa mechi
kati ya Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8 mchana wakati saa 10
jioni ni AFC ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
Mei 11
mwaka huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na Magereza ya Iringa wakati
Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe zitaumana kuanzia saa 10
jioni.
Simiyu
United ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza kucheza saa 8 mchana
katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Saa 10 jioni ni
mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars FC.
Jumapili
(Mei 11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida United (Singida) na
Mbao FC ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni pambano kati ya mabingwa
wa Mkoa wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita Veterans FC ya Geita.
Hata hivyo Kutokana na marekebisho yanayofanyika katika Uwanja wa Sokoine kwa
ajili ya ukaguzi wa CAF. Mechi za RCL za kituo cha Mbeya sasa zitachezwa
kwenye Uwanja wa CCM Vwawa uliopo Mbozi mkoani Mbeya.
Ligi
hiyo itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza kila kundi itapanda
daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015.
MAKOCHA NGORONGORO HEROES,
EAGLES KUTETA
Makocha
wa timu za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na Nigeria (Flying
Eagles), Manu Garba wanakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati yao kwa
ajili ya mechi ya Jumapili.
Mkutano
huo utafanyika kesho (Mei 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia saa 5 kamili asubuhi.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 20 itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa 10 kamili jioni katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Fainali
hizo za 19 za Afrika zitafanyika mwakani nchini Senegal zikishirikisha timu
saba zitakazofuzu kwenye mechi za mchujo, na Senegal wanaoingia moja kwa moja
kutokana na kuwa wenyeji.
Wakati
Ngorongoro Heroes leo (Mei 9 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi yake
Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Flying Eagles yenyewe muda huo huo itafanya mazoezi
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa sh.
5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
EmoticonEmoticon