Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo
kutoka kwa Mhandisi wa ujenzi wa Daraja la Mbutu kata ya Butu Wilayani
Igunga Bw Christopher Makoye wakati alipokagua ujenzi wa daraja hilo
ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu kwa wananchi wanaounganishwa na
kuptia daraja hilo, Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu
ya Tabora, Manyara na Singida akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali
na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Ujenzi wa daraja
hilo unagharimu jumla ya shilingi Bilioni 13 za Tanzania linatarajiwa
kukamilika hivi karibuni,Wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa
NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Tabora Bw. Hassan wa Kasubi.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati aishiriki katika ujenzi wa daraja hilo. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
mhandisi wa ujenzi wa daraja la mto Mbutu Bw. Christopher Makoye wakati
alipokagua ujenzi wa daraja hilo. Mafundi wakienelea na ujenzi Mafundi wakiwa kazini Moja ya eneo la daraja hilo lilikwa limesukwa nondo. Mkuu
wa wilaya ya Igunga Bw. Elibariki Kingu akizungumza na vyombo vya
habari katika eneo hilo la ujenzi mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kukagua ujenzi wa daraja hilo.
EmoticonEmoticon