Kiungo
mshambuliaji wa timu ya Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amewasili
nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya
michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe.
Kazimoto
ambaye amewasili nchini jana (Mei 5 mwaka huu) anatarajia kusafiri leo
(Mei 6 mwaka huu) kwenda Tukuyu mkoani Mbeya ambapo Taifa Stars imeweka
kambi yake chini ya Kocha Mart Nooij kujiandaa kwa mechi hiyo.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager juzi (Mei 4 mwaka
huu) ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi (Flames) ikiwa ni sehemu ya
maandalizi kabla ya kuikabili Zimbabwe (Mighty Warriors). Mechi hiyo
dhidi ya Flames ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na kumalizika
kwa suluhu.
EmoticonEmoticon