Kamishina wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi , Ajira na Watu Wenye Ulemavu , Suzan Mkangwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi kutoka Mgodi wa Barrick North Mara, Michael Bernard (wa kwanza kulia) , alipotembelea banda la Barrick North Mara kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema Mkoa wa Njombe
Baadhi ya wanafunzi wakipata mafunzo ya kudhibiti majanga ya moto katika maonesho haya yanayoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema Mkoa wa Njombe
Katika kuhakikisha jamii inakuwa salama, migodi ya Barrick nchini ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa inatumia maonesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi yanayoendelea kwenye viwanja Mji Mwema katika halmashauri ya wilaya ya Njombe kutoa elimu ya Afya na Usalama kupitia programu yake ya ‘Journey to Zero’ yenye lengo la kutokomeza vitendo hatarishi kwa usalama wa wananchi.
Maonesho ya Afya na Usalama mahali pa kazi ambayo hufanyika kila mwaka huandaliwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) na kauli mbiu ya mwaka huu ni Mazingira Bora ya Kazi Kisaikolojia ni Njia ya Kuimarisha Ustawi wa Wafanyakazi na Kujenga Taasisi Imara.
Akielezea jinsi kampuni inavyotekeleza sera za Usalama, Afisa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi , kutoka Mgodi wa Barrick North Mara, Michael Bernard, amesema kupitia maonesho haya wananchi wa Mkoa wa Njombe na vitongoji vyake wanapata fursa ya kujifunza kanuni za usalama na kuona vifaa vya kisasa vinavyotumika kuwezesha uwepo wa usalama kwenye migodi ya Barrick.
“Mgodi wa Barrick North Mara unayo mitambo ya kisasa ya uchimbaji ambayo inahakikisha usalama wa mfanyakazi na vifaa vya kitekinolojia ya kupambana ajali maeneo ya kazi,” ameongeza.
Kwa Upande wake , Afisa Mwandamizi Usalama na Afya kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Beatus Yusto Lujegi alisema kwamba moja ya sera kubwa ya mgodi ni kutokomeza madhara (Journey to Zero) kwamba pamoja na shughuli za uchimbaji mfanyakazi anapoingia na kurudi nyumbani lazima awe salama.
Amesema pamoja na mambo mengine mgodi wa Barrick Bulyanhulu unatumia vifaa na mitambo ya kisasa kabisa kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na uchechuaji wa madini kwa kutumia teknolojia ya juu kabisa.
Naye Wilson Luther Kingu, Afisa usalama kutoka Mgodi wa Barrick Buzwagi amesisitiza kwamba pamoja na mgodi kuwa katika hatua za ufungaji lakini bado wanahakikisha usalama wa wafanyakazi wakati ufungaji unapewa kipaumbele.
Wananchi wanaotembelea banda la maonesho la migodi ya Barrick wanaendelea kushuhudia inavyotekeleza kauli mbiu ya mwaka huu kwa vitendo na kupatiwa maelezo jinsi kampuni kupitia programu yake ya Journey to Zero inavyofanikisha kuwepo usalama kwa wafanyakazi wake, jamii nzima na utunzaji wa mazingira.
Wananchi pia wanajionea vifaa vya teknolojia ya kisasa vya kuwezesha usalama Mahali pa kazi na majumbani pia wananchi wanapata fursa ya kufundishwa masuala ya usalama , utunzaji wa mazingira na udhibiti wa majanga ya moto.
Usalama ni suala ambalo kampuni ya Barrick inalipa kipaumbele kikubwa na ndio maana imeandaa programu mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia maonesho haya lengo kubwa likiwa ni kutokomeza vitendo hatarishi kwa usalama wa wananchi.
Hili kufanikisha suala hili ni jukumu ni jukumu la kila mmoja kuzingatia kujilinda na kuwalinda wenzake sambamba anapinga na kukemea matukio yanayoweza kusababisha matukio ya ajali.
Kamishina wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi , Ajira na Watu Wenye Ulemavu , Suzan Mkangwa akipata maelezo alipotembelea banda la Barrick North Mara kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema Mkoa wa Njombe
Kamishina wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi , Ajira na Watu Wenye Ulemavu , Suzan Mkangwa akipata maelezo alipotembelea banda la Barrick North Mara kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema Mkoa wa Njombe
Baadhi ya wanafunzi wakipata mafunzo ya kudhibiti majanga ya moto katika maonesho haya yanayoendelea

Baadhi ya wanafunzi wakipata mafunzo ya kudhibiti majanga ya moto katika maonesho haya yanayoendelea
Wageni na wananchi wa Mkoa wa Njombe wakipata mafunzo kwa vitendo jinsi ya kukabiliana na majanga baada ya kutembelea Banda la Barrick kwenye maonesho yanayoendelea ya Usalama Mahali Pa Kazi Mkoani Njombe
Wageni na wananchi wa Mkoa wa Njombe wakipata maelezo kwenye Banda la Barrick
Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wananchi walipotembelea Banda la Barrick
Wageni na wananchi wakitembelea banda la Barrick North Mara kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema Mkoa wa Njombe
Wageni na wananchi wakitembelea banda la Barrick North Mara kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema Mkoa wa Njombe











EmoticonEmoticon