Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameitaka TIRDO kushirikiana na Taasisi zingine kuhakikisha watanzania wanapata nishati safi rafiki na Kwa bei rahisi .
Mhe. Rais ametoa agizo hilo katika Kongamano la Kitaifa la Mama na Baba Lishe lililofanyika katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar es salaam .
Katika Maonesho hayo TIRDO imeshiriki Kwa kuonesha Teknolojia ya kuzalisha mkaa kwa kutumia mabaki ya bidhaa za kilimo kama pumba za mpunga ,vifuu vya nazi ,maganda ya chikichi pamoja mchanganyiko wa vifuu na Pumba za mpunga.
Mtaalam na Mtafiti wa Nishati Mhandisi Augustino Masse ameeleza kuwa katika maonesho haya wamewafikia wadau wengi na kutoa elimu juu ya dhana ya matumizi ya nishati bora ya kupikia .
Mhandisi Masse ameeleza kuwa Ili kukamilisha mzungumo mzima wa nishati safi ni lazima kuzingatia vitu vitatu ambavyo ni nishati ,jiko linalotumika tabia ya mpishi ,Mhandisi Masse anaeleza kuwa bila hizo hatua tatu kuzingatiwa bado dhana ya nishati safi na rahisi haitokamilika .
Katika kuhitimisha maonesho hayo ,Mhe. Rais ametoa agizo Kwa Mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha Mama Lishe wanapatiwa maeneo rafiki Kwa biashara zao ,kupewa miundombinu rafiki na pia taasisi za kifedha kuja Mikopo rahisi itakayowafaa Mama na Baba lishe kulingana na Mazingira yao ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe mfano wa hundi ya Shilingi bilioni 94.158,250,400/= kwa ajili ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.













EmoticonEmoticon